Alain Robert ni raia wa Ufaransa ambaye anajulikana ulimwenguni kwa kupanda majengo marefu. Hivi karibuni alivunja record yake mwenyewe kwa kupanda Jengo refu kulko yote duniani la Burj huko dubai likiwa na urefu wa 828-metre (2,717-foot).

Hata hivyo baada ya kupanda Alain alikaririwa na Reuters akisema kuwa haofii kufa kwani kupanda majengo marefu ni sehemu muhimu ya maisha kwake kama ilivyo kula au kuvuta pumzi, “My biggest fear is to waste my time on earth. For me, climbing is as important as eating and breathing. Climbing skyscrapers is my lifetime love and passion” Robert said.

Robert kwa mara ya kwanza alipanda jengo la ghorofa nane akiwa na umri wa miaka 12 baada ya kusahau funguo zake huko, tangu hapo aliona kuwa huo ni sehemu ya mchezo wake na amesha wahi kupanda majengo zaidi ya 100 duniani likiwemo la Petronas Twin Towers la Malaysia mwaka jana. (Gonga hapa uisome).

Mengine ni Taiwan’s Taipei 101 lenye ghorofa 101, mnara wa the Eiffel Tower huko Ufaransa France, the Empire State building huko New York na the Sears Tower huko Chicago.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA