TANZIA ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI SHINYANGA ALOYSIUS BALINA AMEFARIKI DUNIA


Mhashamu Askofu wa kanisa la Katoliki jimbo la Shinyanga mjini Aloysius Balina amefariki dunia leo asubuhi majira ya saa tano katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza alikokuwa akipatiwa matibabu.

Akithibitisha taarifa hizi Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Bugando Dr. Charles Majinge amesema kuwa "Ni kweli Mhashamu Baba Askofu Balina amefariki majira ya saa tano asubuhi ya leo na alikuwa amelazwa hospitalini hapa akitibiwa kutokana na kusumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa kansa"

Marehemu Mhashamu Baba Askofu kabla ya kuwa askofu wa jimbo katoliki Shinyanga alikuwa Askofu wa kwanza wa jimbo Katoliki la Geita kabla ya kuhamishiwa jimbo kuu la Shinyanga.

Taratibu za mazishi na taarifa zaidi zitatolewa na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hivyo waumini wanataarifiwa kuwa watulivu kwa kipindi hiki na kumwombea marehemu wakati tukisubiri kutangazwa rasmi.

Bishop Aloysius A. Balina alizaliwa june 21st 1945 katika mji wa Isoso, Ntuzu wilayani Bariadi; na kupewa daraja la U-Askofu tarehe 06 January 1985

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA