HABARI MPYA KWA WATUMIAJI WA WHATSAPP SASA UTAWEZA KUPIGA NA KUPOKEA SIMU

Baada ya facebook kuinunua Whatsapp, kumekuwa na mabadiliko ya features mbalimbali  katika kuiboresha App hii kuwa bora zaidi duniani kwa kukidhi mahitaji ya watumiaji. Mwezi uliopita walianzisha uwezo wa kujua kama mtu uliyemtumia ujumbe kama ameupata na kuusoma kabisa kwa kubadili alama za tick na kuwa za blue. 

Wataalam wa mtandao huu wameendelea kugundua na kuongeza features zingine, wakati huu wako katika majaribio ya mtumiaji wa whatsapp kuweza kupiga simu na kupokea simu kutoka kwa mtumiaji mwingine anayetumia pia app ya whatsapp



Majaribio ya huduma hii ya kupiga na kupokea simu kwa kutumia whatsapp yameanza huko Uholanzi na kuchukua screenshot hii ya majaribio. Tegemea hivi karibuni kuanza kupiga simu kwa kutumia whatsapp

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA