DEUTSCHE WELLE (DW) KUTUMIA MBINU MPYA YA KUKUFIKISHIA TAARIFA MOJA KWA MOJA KUPITIA WHATSAPP
Mpenzi
msikilizaji, msomaji na shabiki wa DW popote pale ulipo, unasemaje
kuhusu kupokea habari, picha, vidio na sauti zenye ujumbe wa
kukuchangamsha moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi?
DW
inakupa huduma hii mpya bila malipo kupitia mtandao wa WhatsApp.
Unachohitaji ni simu yako tu yenye huduma ya intaneti na pia WhatsApp.
Baada ya hapo fuata hatua zifuatazo kupokea taarifa kutoka kwetu:
1. Hifadhi namba ya WhatsApp ya Idhaa ya Kiswahili ya DW ambayo ni +4915752862185 kwenye simu yako
2. Tuma ujumbe kwa kutumia WhatsApp kwenye namba hiyo ukiwa na neno “Niunge.” Ukipenda, tuambie jina na pia nchi yako.
Baada
ya hapo, tutakuweka kwenye orodha ya watu wanaopokea ujumbe kutoka
kwetu kila tunapotuma taarifa mpya. Usihofu, hatutakutumia zaidi ya
taarifa mbili kwa siku.
Kuwa
mmoja wa wanachama wetu wa mwanzo kabisa kwenye jamii ya DW WhatsApp,
uwe karibu kabisa na habari mpya na ujumbe wa moja kwa moja kwenye simu
yako. DW iko nawe popote ulipo.
Mueleze
na rafiki yako kwa kumtumia namba yetu ya simu. Unaweza pia
kutufahamisha vile ambavyo ungelipenda kutumia WhatsApp kupokea habari
na kututumia ujumbe wa moja kwa moja.
Ikiwa
bado wewe hujaanza kutumia WhatsApp na ikiwa simu yako inaweza kutumia
huduma hiyo, tafadhali weka sasa kwa simu zinazotumia mifumo ya Android,
BlackBerry, Windows, ingia kwenyehttp://www.whatsapp.com/download/.
Usalama
wa Taarifa: Namba yako ya simu itatumiwa na DW tu. Usalama wako wakati
tunapotumia taarifa zako ni muhimu kwetu. Tunazitumia tu kwa mujibu wa
matakwa ya kisheria. Kwa taarifa zaidi juu ya usalama wa taarifa za
WhatsApp, tembeleahttp://www.whatsapp.com/legal/.
mjengwablog.
Comments
Post a Comment