TECHNOLOGY: JIFUNZE NJIA BORA YA KUWASILIANA KWA SAUTI KUPITIA FACEBOOK MESSENGER

Technolojia inazidi kubadilisha maisha kila siku na kufanya gharama za mawasiliamo kuwa rahisi zaidi, kwa wale watumiaji wa simu zenye mfumo wa uendeshaji (operating system) katika simu zao kama iOS au Android sio wageni kusikia neno kama Viber, WhatsApp, Tango, Telegram, Skype,Hangouts,Kik,BBM na nyingine nyingi.

Hizi Apps zote dhumuni lake ni katika kuwasiliana kwa njia ya maneno, picha, na video na baadhi ya Apps nyingine kuwekea kitu cha ziada ambacho kinazitofautisha na Apps zingine kama  uwezo wa kutuma document kama BBM au kupiga simu kupitia App hiyo mfano Viber, Skype, Facebook Messanger. 
Application zote hizi za simu zinapatikana katika soko linalojulikana kama Android Marketplace maarufu kama Play store au kwa jina linkine "Google play"  na iOS App store maalumu kwa simu kama iphone.

Leo ningependa kuzungumzia zaidi application inayoitwa "Facebook Messenger' iliyozinduliwa kwa majaribio  August 9, 2011 kwa matumizi ya  iOS na Android ikaanza matumizi rasmi  December 2012, kwa baadhi ya nchi kama Australia, India, Indonesia,USA, South Africa,na Venezuela ambapo ikawapa uwezo watumiaji wake kutumia facebook messenger hata bila kuwa na account facebook bali ikawezesha kutumia namba ya simu pekee.
 
Logo ya Facebook Messenger.
Facebook Messenger ina upekee wa aina yake kwa wale watumiaji wa facebook wanaweza kuchat kwa maneno,picha,video na kumpigia simu na kuongea moja kwa moja bila kuwa na mikwaruzo ya kukata kata hata kama internet inakuwa inatumia 2G.

Application hii inarahisisha gharama za mawasiliano kwa kiasi kikubwa hasa kwa wale wenye ndugu waishio ughaibuni,hata hapa nyumbani Tanzania.Utofauti wake na App kama viber au skype mara nyingi kusikilizana inakuwa ngumu sana na mikwaruzo ya hapa na pale pia inahitajika internet yenye kasi sana, wakati mwingine unaweza kuta unatumia 3G lakini bado ikawa ni shida katika kusikilizana vizuri. 

Jinsi ya kutumia facebook Messenger.
Download kupitia play store, baada ya hapo install  kwenye simu yako, ifungue mara baada ya kuingiza katika simu yako, tafuta watu walio katika chat room yako  katika kila jina utaona alama MBILI zinazotofautiana ya kwanza ni "F" yaani facebook  hiyo achana nayo, ukiona hivyo ujue huyo rafiki hana application hiyo kwenye simu yake, pindi utakapoona alama kama hiyo hapo juu kwenye picha ndio halisi ya facebook Messenger fungua kama unataka kumtumia ujumbe kwa juu utaona alama ya simu ya rangi ya blue, bofya hapo kwenye alama ya simu kuruhusu kupiga simu itaanza kuita.



Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA