KOREA KASKAZINI NA BOMU NA HYDROGEN

Tangazo kuhusiana na jaribio hilo la bomu la Hydrogen la Korea Kaskazini
Siku moja baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la bomu la nyuklia aina ya Hydrogen, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekubaliana kuanza mikakati ya kuiwekea vikwazo kufuatia jaribio hilo.
Hata hivyo baadhi ya Wataalam wameonyesha kuwa na wasi wasi kuhusu jaribio la sasa la Nyuklia la Korea Kaskazini ambalo ni la nne katika muongo mmoja kwamba nguvu yake inaweza kuwa ni bomu la hydrogen.
Kwa faida yako tu bomu la hydrogen ni moja ya mabomu hatari ya jamii atomic au nyuklia yenye nguvu zaidi. Wataalam wanasema bomu hili la hydrogen lina uwezo mkubwa kiasi kwamba linaweza kulipua mji mmoja wote kwa mlipuko mmoja.
Kufuatia jaribio hilo jamii ya kimataifa imendelea kulaani tukio hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Waziri wa zamani wa Mambo ya nje ya Korea Kusini Ban Ki moon yeye amesema jaribio hilo la bomu la nyuklia ni hatua ya kuogopesha.
"Hili jaribio kwa mara nyingine limekiuka maazimio kadhaa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na wito wa pamoja wa Jamii ya kimataifa kukomesha vitendo hivyo. Pia linakwenda kinyume kabisa na utamaduni wa kimataifa wa majaribio ya mabomu ya nuclear. Tendo hilo linaonekana ni la kuogopesha kwa usalama wa kanda na kupuuza juhudi za kimataifa za kuacha kutengeza. Ninalaani kwa nguvu jambo hilo."
Huko Marekani nayo Ikulu ya White house imesema utafiti wake wa awali kuhusu jaribio hilo la bomu nyuklia la Korea ya Kaskazini haufanani na madai kwamba nchi hiyo imefanikiwa kulipua bomu la Hydrogen.
Msemaji wa White house Josh Earnest amesema kutengwa kwa Korea ya Kaskazini unapaswa kuimarishwa zaidi kama itaendelea na matendo yake ya ukiukaji ikiwa ni pamoja na kufanya majaribio ya makombora ya angani.
"Tumesikitishwa sana na matokeo ya uharibifu wa amani na utulivu baada ya matendo ya ukiukaji wa Korea Kaskazini kuzidi kuongezeka. China na Urusi nao pia wamesikitishwa . Ndio maana tunafanya bidii kuiweka pamoja jamii ya kimataifa na kuweka wazi kwa Korea Kaskazini kwamba njia ni moja tu iliyobaki ambayo ni nzuri kwa raia wa Korea Kaskazini, ambayo itakuwa nzuri kwa uchumi wa Korea kaskazini, nzuri kwa nchi Korea kaskani kwa maana ya uwezo wao wa kujihusisha na jamii ya kimataifa."BBC

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA