Posts

Flaviana Matata & Hasheem Thabeet named Russel Simmons' D.E.F Africa Ambassadors

Image
Teddy Kalonga-Haight | Hasheem Thabeet | Flaviana Matata The Diamond Empowerment Fund™ (D.E.F.), an independent organization founded in 2007 by Russell Simmons and members of the jewelry industry, is pleased to recognize Flaviana Matata, former Miss Universe Tanzania as D.E.F.'s new Africa's Angel Ambassador as well as NBA player for the Memphis Grizzlies Hasheem Thabeet as D.E.F.'s new Athlete for Africa Ambassador. In her first assignment, Flaviana visited with students at African Leadership Academy and CIDA City Campus in South Africa in the spring, and blogged about her experience for D.E.F. Flaviana intends to blog for D.E.F.'s website and Facebook page regularly, acting as a correspondent for D.E.F. in sharing the stories of the students at the programs D.E.F. supports. In his role, Hasheem will develop a program with D.E.F. to help raise awareness and support for the cause of empowerment through education for Africa, which will also highlight his is philanthropi

Ilianza Mara, ikaenda Kilimanjaro sasa ni Iringa...

Watu wasiofahamika wakazi wa kijiji cha Igowole wilayani Mufindi mkoani Iringa wamechoma moto ofisi ya Serikali ya kijiji hicho na moto huo umeunguza nyaraka zote za kijiji hicho toka kilipoanzishwa hadi sasa. Wakizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari juu ya tukio hilo, wakazi wa kijiji hicho wanadai kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumanne na kuwa jitihada za wananchi kuzima moto huo zilikwama baada ya moto huo kuongeza kasi kila wanapojaribu kuzima. Pia walisema kinachoonekana katika tukio hilo ni hujuma kutokana na siku za hivi karibuni wananchi wa kijiji hicho kufanya maandamano kupinga mwenendo wa viongozi wa Serikali ya kijiji hicho kwa hatua yao ya kuuza mali za wananchi pamoja na zile za kijiji bila kuwashirikisha malalamiko ambayo yalifikishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi na kuundiwa tume ambayo hadi sasa majibu na hatua haitatolewa kwa wahusika jambo linalotajwa kuwatibua zaidi wananchi hao. Picture YATOKANAYO Kwa mbayuwayu mwenye akili yake, baada

Poleni sana wapenzi wa blog yangu

Napenda kuwapa pole wapenzi wa blog hii kwa kukosa Habari kwa muda wa siku kadhaa kama wiki moja hivi,mwanablog wenu nilikuwa naumwa lakini namshukuru Mungu nimerejea tena na mambo yanaendelea kama kawaida na nitaendelea kuwashushia habari kama kawaida.

AY ashinda tuzo za MUSEKE

Image
Mwanamuziki Ambwene Yesaya aka AY, ameshinda kwenye kinyanganyiro cha Museke Online Africa Music Awards (MOAMAs) Award. Award hii imeandaliwa na wavuti wa www.museke.com ikiwa na dhamira ya kutambua vipaji na kazi za wanamuziki wa Afrika waliofanya vizuri kwa mwaka 2009/10. AY alikuwa kwenye kundi la East Africa Song of the Year. Hayo yamethibitishwa na AY mwenyewe kupitia status ya mtandao wa facebook “M happy:Nimeshinda Awards za Museke:East African Song of the Year (LEO)..mafans wangu nawashukuru sana coz mnafanya mambo kwa vitendo na matokeo yanaonekana..tonight nitaparty na watu wangu wa Kampala.Muuuuuuch RESPECT Brothers N’ Sistaz” alisema AY akiwaambia mashabiki wake.

Serikali yawaonya wenye 'blogs'

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Clement Mshana amewataka wamiliki wa mitandao ya habari maarufu kama 'Blogs' na wale wa magazeti ya udaku kuacha mara moja kuweka picha na habari zinazodhalilisha jamii. Akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa wanahabari mjini Morogoro, Mshana alisema Tanzania imekuwa na ongezeko kubwa la vyombo vya habari tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi. "Hilo ni jambo zuri katika kutoa habari za kuwaelimisha, kuwaburudisha na kuwahabarisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali yakiwamo ya afya, siasa, maendeleo na ustawi wa jamii kwa ujumla hasa pale habari hizo zinapokuwa zimeandikwa kwa ufasaha bila udhalilishaji. "Lakini utakuta katika blog, badala ya kuwekwa habari na picha za kuelimisha jamii, zinawekwa picha za watu wakiwa uchi! Huku ni kuwadhalilisha watu. Ijulikane kuwa mitandao hiyo husomwa pia na watoto wadogo, hii inawafundisha nini?" alihoji Mshana. Hata hivyo, alisema si magaze

FACEBOOK MAKE COMMUNICATION EASIER FOR EVERYONE INTRODUCED VIDEO CHART

Image
Video, audio, and text chat with your friends - Have them talk to you right from Video Chat on your profile. If they have Video Chat too, just have them click 'Talk to me' under your profile. Invite friends who also have Video Chat right into the conversation from the Video Chat application. Schedule times for you and your friends to meet up at your chat room. You can share YouTube videos and watch them with your friends by sending a YouTube URL to your friends in the text chat window. The YouTube video starts playing in a new window in the application. Your friends can record new audio and video messages for you when they come looking for you and if you are not present in your room. You friends can also view messages left for you in your room. You are alerted on your instant messenger of choice when someone visits your room. Your visitors can send you a personalized text message that you will receive on your instant messenger when someone visits your widget. You can click on t

Brazili kucheza na Taifa Stars ya Tanzania Juni 7 05/27/2010

Image
Brazili kucheza na Taifa Stars ya Tanzania Juni 7 05/27/2010 Timu ya soka ya Brazili ambayo imeshawasili nchini Afrika Kusini tayari kwa mashindano ya kuwania Kombe la Dunia la Soka, inatarajiwa kuingia nchini Tanzania Juni 5 kwa ajili ya mechi ya kirafiki na Timu ya soka ya Tanzania ya Wanaume, Taifa Stars hapo Juni 7, 2010. Balozi wa Brazili nchini Tanzania, Francisco Carlos Soares Luz amesema timu hiyo itawasili na nyota wake wote watakaoshiriki katika fainali hizo.

NITASOMA SCHOLARSHIP WINNERS MAY 2010

Image
RENILDA AMBROSE CHIMA FULL DURATION SCHOLARSHIP CHIMALA HIGH SCHOOL MBEYA Other winners include; 1.SUSAN MILANZI NITASOMA LAPTOP 2 2.JOYCE MARUWA NITASOMA STATIONERY INSTITUTE OF SOCIAL WORK (HRM) 3RD YEAR 3. SAADA S SADALA NITASOMA MOBILE T.I.A BBA 1ST YEAR

MACHOZI BAND WAAMISHA ,MAKAZI TO MZALENDO PUB KILA FRIDAY

Image
GOOD NEWS KWA WAPENZI WA MACHOZI BAND IJUMAA HII.......KIWANJA KITAKUWA MZALENDO PUB EVERY FRIDAY Machozi Band sasa wamehamia mzalendo pub sehemu yenye upepo wa asili wa kutosha bila kuhitaji mafeni.......... Ni Mzalendo Pub, kuanzia Ijumaa ya tar 28 May 2010 na Ijumaa nyingine zote zitakazofuata Karibuni mu enjoy, na samahanini tena kwa kuwakosesha burudani Ijumaa iliopita Alhamisi ni Savannah Lounge kama kawaida na Jumapili ni Thai Village

Tiketi za WOZA 2010 kwa Tanzania zawasili

Image
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Florian Kaijage kizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusiana na utaratibu wa kupata tiketi zilizoletwa na FIFA ili kushuhudia baadhi ya michezo ya Kombe la Dunia. Kwa sababu za kiusalama na uthibitisho, watu wote walionunua tiketi hizo wanahitajika kuwa na risiti zao pamoja na picha ndogo 'Passport Size' ili waweze kupatiwa tiketi zao

Wafanyakazi WOTE wa ATCL waachishwa kazi

Image
Kamati ya kudumu ya Bunge na Fedha na Uchumi iliyokutana jijini Dar Es Salaam tarehe 25 Mei 2010 imeridhia mapendekezo na ushauri wa Ofisi ya Msajili wa Hazina la kuwaachisha kazi Wafanyakazi wote wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ili kuipunguzia mzigo Serikali. Ushauri huo umetolewa na mshauri wa Msajili wa Hazina bwana Godfrey Msella na kusema, "kama ATCL haibebeki, ni bora Serikali ibwage manyanga" na hivyo kufuatiwa na tamko rasmi la Mwenyekiti wa tume hiyo ya Bunge, mhe. Abdallah Kigoda. Hatua kama hiyo iliwahi kuchukuliwa katika shirika la Bima la Taifa (NIC) na imependekezwa kuwa hatua hii isiichie ATCL pekee bali ifike pia katika Shirika la Reli nchini (TRL). habari hii ni kwa hisani ya tovuti ya www.wavuti.com

TWANGA KUSUGUA KISIGINO MBEYA NA IRINGA.

Image
Bendi ya muziki wa Dansi ya African Stars maarufu kama Twanga Pepeta iliyo na maskani yake jijini Dar, inatarajiwa kufanya ziara maalum katika mikoa ya Iringa na Mbeya ili kuwashukuru mashabiki wa mikoa hiyo miwili kutokana na kuipigia kura kwa wingi na kufanikiwa kuchukua tuzo tatu za KILI kwa mwaka huu. Ziara hiyo inatarajiwa kuanzia katika Mkoa wa Iringa siku ya Alhamisi ya tarehe 3 mwezi wa sita katika Club ya V.I.P, na siku inayofuata ya tarehe 4 mwezi wa sita Twanga pepeta itamalizia ziara yake katika ukumbi wa Mkapa uliopo katikati ya Jiji la Mbeya. Maonyesho yote mawili yanatarajia kuanza saa mbili za usiku na kwa Mkoa wa Iringa, Twanga pepeta inataraji kusindikizwa na Bendi ya Sweat Noise iliyo na maskani yake Iringa. Twanga pepeta itaitumia ziara hiyo ya mikoa ya Iringa na Mbeya kuwadhihirishia mashabiki wa Mikoa hiyo kwamba Twanga Pepeta iko juu na wanataraji kusafiri na kikosi kizima kilicho na nyota wote wakiongozwa na Kiongozi Mkuu mamaa Luiza Mbutu na wengineo kibao. Aid