AY ashinda tuzo za MUSEKE



Mwanamuziki Ambwene Yesaya aka AY, ameshinda kwenye kinyanganyiro cha Museke Online Africa Music Awards (MOAMAs) Award.

Award hii imeandaliwa na wavuti wa www.museke.com ikiwa na dhamira ya kutambua vipaji na kazi za wanamuziki wa Afrika waliofanya vizuri kwa mwaka 2009/10.

AY alikuwa kwenye kundi la East Africa Song of the Year.

Hayo yamethibitishwa na AY mwenyewe kupitia status ya mtandao wa facebook “M happy:Nimeshinda Awards za Museke:East African Song of the Year (LEO)..mafans wangu nawashukuru sana coz mnafanya mambo kwa vitendo na matokeo yanaonekana..tonight nitaparty na watu wangu wa Kampala.Muuuuuuch RESPECT Brothers N’ Sistaz” alisema AY akiwaambia mashabiki wake.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA