Ilianza Mara, ikaenda Kilimanjaro sasa ni Iringa...

Watu wasiofahamika wakazi wa kijiji cha Igowole wilayani Mufindi mkoani Iringa wamechoma moto ofisi ya Serikali ya kijiji hicho na moto huo umeunguza nyaraka zote za kijiji hicho toka kilipoanzishwa hadi sasa.

Wakizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari juu ya tukio hilo, wakazi wa kijiji hicho wanadai kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumanne na kuwa jitihada za wananchi kuzima moto huo zilikwama baada ya moto huo kuongeza kasi kila wanapojaribu kuzima.

Pia walisema kinachoonekana katika tukio hilo ni hujuma kutokana na siku za hivi karibuni wananchi wa kijiji hicho kufanya maandamano kupinga mwenendo wa viongozi wa Serikali ya kijiji hicho kwa hatua yao ya kuuza mali za wananchi pamoja na zile za kijiji bila kuwashirikisha malalamiko ambayo yalifikishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi na kuundiwa tume ambayo hadi sasa majibu na hatua haitatolewa kwa wahusika jambo linalotajwa kuwatibua zaidi wananchi hao.
Picture
YATOKANAYO

Kwa mbayuwayu mwenye akili yake, baada ya kuambiwa haya kisha achanganye na akili yake, hana budi kukemea yaliyotokea kisha kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa tukio kama hili halitokei, si katika kijiji hicho tu bali kwa nchi nzima.

Mbayuwayu mwenye akili pia yampasa kutafuta chanzo na akitake chanzo kwa minajili ya kutatua tatizo toka katika kina. Aifahamu kinagaubaga sababu ya wananchi kuishiwa uvumilivu na subira. katika kero na dukuduku zao wanazoziwaklisha kwa watendaji. Wananchi wamekuwa watiifu sana na kufuata maelekezo ya viongozi wao, lakini inavyoelekea, imefika mahali utii umepungua kama si kutoweka kabisa. Sababu ni ipi sana? Pengine wamekosa majibu ya kuridhisha. Pengine wameishia kupewa ahadi hewa. Pengine kero walizoziwakilisha hazipati ufafanuzi kwa muda muafaka. Pengine wamechoka na maneno yasiyo tija. Ni mengi na sababu ni nyingi lakini Kiongozi safi atadadisi apate kuufahamu ukweli; lengo lake likiwa ni kushughulikia chanzo cha uzembe uliojitokeza na kuzuia hali hiyo kutokujirudia tena.

Wahenga waliasa kuwa dalili za mvua ni mawingu na usipouziba huo ufa unaochomoza, basi mvua itakaponyesha uwe tayari kuujenga ukuta, sasa sjui kama umeshahesabu gharama ukajua kama ni vyema kuziba ufa au kujenga ukuta mzima. Mwenye macho haambiwi tazama. Linalowezekana leo, lisingoje kesho!

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA