Kanisa Katoliki latoa tamko kuhusu Dkt. Slaa
KANISA Katoliki limekuja juu na kukanusha tuhuma zinazoelekezwa kwa kanisa hilo kuwa limemtuma Dkt. Willibrod Slaa kuwania urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu. Vile vile kanisa hilo limesema kuwa Kanisa Katoliki si taasisi inayojihusisha na harakati za kisiasa wala si chama cha kisiasa kinachohusika kwa namna yoyote ile na uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Mhashamu Jude Ruwa'ichi alisema kuwa habari za kanisa hilo kuhusishwa na Dkt. Slaa katika harakati zake za siasa zimelenga kulichafua kanisa na kulipunguzia heshima ndani ya jamii. "Tunapenda Watanzania wenzetu waelewe kuwa Kanisa Katoliki halijamtuma wala halitamtuma mtu yeyote kugombea nafasi ya uongozi kwa jina la kanisa, kwani si jukumu lake...kanisa litaendelea kuhubiri upendo, haki, amani, mapatano na mshikamano na litaendelea kutoa mchango wake n