NHC waanza kuwatimua Wapangaji batili
Shirika la Nyumba ya Taifa (NHC) limeanza kuwaondoa kwa nguvu baadhi ya wapangaji ambao wamebainika kuishi kwenye nyumba hizo kwa kurithishana badala ya kufuata utaratibu maalumu uliopangwa na shirika. Picture Hatua hiyo imewakumba baadhi ya wapangaji katika maghorofa ya Keko Mtaa wa Magurumbasi A ambapo kazi hiyo ilisimamiwa na viongozi wa NHC na Kampuni ya udalali ya Msolopa. Mwandishi wa gazeti la DarLeo alishuhudia mpangaji Pantalelo Mushi akiondolewa vitu vyake ndani ya nyumba chini ya usimamizi wa wajumbe wa nyumba kumi. Ofisa wa NHC, Anneth Natai, amesema kumekuwa na mazoea ya wapangaji kuwarithisha watu wengine bila ya idhini ya uongozi. Kutokana na kitendo hicho, NHC imekuwa ikipatwa na usumbufu pindi kunapotokea tatizo na hata wengine kushindwa kufuata masharti yao. “Kuna wapangaji wengine wamekuwa wakilipa kodi kubwa kwa kuwapa wamiliki halali ambayo hata sisi hatuijui na pia tumekuwa hatuwafahamu wapangaji halisi,” amesema. Amesema kazi ya uondoaji wapangaji wasiotambulika na NHC inaendelea ili kuwabaini na kuwaondosha. “Tunaendelea na kazi hii na wale wote ambao wanalipa kodi kupitia migongo ya watu tutawaondoa kwenye nyumba hata hivyo kila mtu ana haki ya kupanga ispokuwa afuate masharti na tabia ya kurithishana haipo isipokuwa kila mmoja anatakiwa kufuata taratibu,”amesema. source Dar Leo
Comments
Post a Comment