BIG BROTHER AFRICA 2010 KUANZA KESHO

Lile shindano maarufu la Big Brother Africa kwa mwaka huu wa 2010 linatarajiwa kuanza rasmi Jumapili kesho tarehe 18 Julai 2010 huko Johanesburg nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kampuni ya MultiChoice Tanzania, jumla ya washiriki 14 watatambulishwa siku hiyo wakati wakiingia katika Jumba la Big Brother. Shindano hilo litadumu kwa siku 91.

Mshindi wa Big Brother 2010 anatarajiwa kuondoka na kitita cha US Dollars 200,000. Kama kawaida shindano hilo litakuwa likirushwa hewani kupitia kituo cha DStv-Channel 198.

Tangu shindano hilo lianzishwe,kumekuwa na maoni tofauti tofauti kuhusu faida au hasara za shindano kama hilo.Wapo watu ambao wamekuwa wakidai kwamba shindano hilo linachangia katika kuporomoka kwa maadili kutokana na vitendo vya ki-ngono ngono vinavyofanywa na washiriki wa shindano hilo.

Pamoja na hayo,shindano hilo limekuwa likijipatia mashabiki na wafuasi chungu mbovu kila mwaka. Mwaka jana Tanzania iliwakilishwa na mmoja wa washiriki wa Miss Tanzania miaka ya nyuma, Elizabeth Gupta, ambaye alitokea kuwa miongoni mwa washiriki wenye mvuto katika jumba hilo.

Je ni nani ataiwakilisha Tanzania katika shindano la mwaka huu?Atakuwa wa jinsia gani? Stay tuned.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA