Mchungaji agoma kuzika majambazi

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), amekataa kushawishika amzike Kikristo moja ya Majambazi kati ya wawili waliyouawa na Jeshi la Polisi na kukaa kwenye jokofu la Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa siku saba.

Jambazi hilo linalojulikana kwa jina la Gerald Machange (26), na lenzie Paulo Yohana (18), ya Chang’ombe mkoani hapo, yaliuawa baada ya kujaribu kuwatoroka Polisi toka kwenye gari yalipokamatwa na vitu walivyokuwa wakiiba kwenye Hotel ya Emirates.


Akiwafariji wafiwa na Waombolezaji nyumbani kwa wazazi wa jambazi Machange, Mchungaji Naftari Njavike wa KKKT Chinangali aliuambia umati uliofurika msibani kwamba, Neno la Mungu linatuasa kuwa, ‘Niangalieni mimi Mkaokolewe’; Lakini watu wameaacha kumuangalia Mungu na badala yake wanaangalia vitendo viovu. “Nawataka mfahamu, Kanisa halina nafasi ya kutetea tabia mbovu za namna hiyo, zinazofanywa kwenye jamii zenye lengo la kuwakosesha amani, utulivu, mshikamano, na tija ya wananchi katika maendeleo yao ya kila siku,” alihubiri Njavike. "Kanisa likifikia kukumbatia na kuwatetea majambazi ambao ndugu wanataka yazikwe kama watu wema wakati walikuwa wanadhulumu na kutishia Usalama wa mali na maisha yao, litakuwa linajiaibisha, na kweli itakuwa haimo kanisani mwake. Msidhani namhukumu; nataka liwe fundisho tusifanye Uovu na kutaka Kanisa lituzike Kikristo kwa Uovu wetu, litadharaulika. Naomba mfahamu, mshahara wa dhambi ni mauti.”

Familia ya marehemu huyo walimwendea mmoja wa Wazee wa kike wa Kanisa la KKKT Chinangali aliyeko mtaa wa Chang’ombe (jina linahifadhiwa) na kudanganya wakiomba afanyiwe mazishi ya Kikristo kwa madai Mzazi wake ni muumini wa usharika, ambapo mchungaji baada ya kujadiliana na uongozi wake wa juu, aligoma kwa kuwa majina ya majambazi hayo hayakuwemo kwenye orodha ya washarika.


Ofisa Upelelezi mkoani Salum Msangi alikiri na kuthibitisha kwamba, Machange na Yohana ni majambazi, walikamatwa katika wizi wakiwa na vitu walivyoiba Hoteli ya Emirates, hivyo ndugu wasiwapotoshe raia wanaojua nini cha kulifanyia ili Taifa waishi kwa usalama, amani, utulivu na mshikamano, huku akimsifu mchungaji kwa kuifungua jamii masikio.

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limempongeza Mchungaji wa Kanisa la KKKT Chang'ombe kwa kukataa kulizika jambazi sugu lililouawa baada ya kukamatwa na vitu vya wizi vilivyoibiwa katika Hoteli ya Emerates.

Ndugu wa marehemu walimjia juu kiongozi huyo wakitaka ajiuzulu kwa madai kuwa amekiuka maadili ya dini.
soma zaidi gazeti la Dar leo

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA