BBA All Star-Mwisho Mwapamba mjengoni tena


Mwisho Mwapamba

BBA All Star Ni habari nyingine
Ilianza Big Brother Africa mwaka 2003, ikaja Big Brother Afrika II (2007), ikaja Big Brother III (2008), baadaye Big Brother Revolution (2209), hata hivyo, zote zinatajwa ni tisa, 10 na itakayofunika ni ya 2010 ambayo inakwenda kwa jina la Big Brother All Stars.

Sababu ambayo inatajwa kuifanya Big Brother mwaka huu kuwa ya kipekee ni uamuzi wa kuwachukua mastaa waliong’ara kwenye fainali zilizopita na kuwapa nafasi ya kuingia tena mjengoni ili kushindana tena.

Tanzania imeshiriki mashindano hayo mara zote, na kufanya vizuri zaidi mwaka 2007, pale Ricahrd Bezuidenhout aliponyakua taji na kujibebea kitita cha Dola za Kimarekani 100 ambazo kwa ‘chenji’ ya wakati huo zilikuwa shilingi 130,000,000. Mwanga wa mafanikio kwa Tanzania kwenye mashindano hayo, ulioneshwa mapema mwaka 2003, pale Mwisho Mwampamba ‘Mr. Morogoro’ aliposhika nafafasi ya pili, nyuma ya Cheris Makubale wa Zambia.

Mwaka 2008, Tanzania iliwakilishwa na Latoya Lyakurwa ambaye aliifanya Tanzania kuwa wa kwanza kutolewa mjengoni kwa awamu hiyo, na Elizabeth Gupta ‘Queen’ alijitahidi mwaka 2009 lakini hakufika mbali, akawa amechomolewa.

Kionjo kikubwa mwaka huu, ni watazamaji kuwaona tena wale mastaa wao waliowakubali kwenye fainali mbalimbali zilizopita, hivyo kuifanya awamu hii ya 2010 kuwa tishio zaidi kuliko zilizotangulia

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA