Posts

SHOW YA DIAMONDS ARE FOREVER YAFUNIKA VIIBAYA VIBAYA MNOOOOO.

Image
DJ Bulla mtamboni akihakikisha show ya Diamond inakwenda sawa kabisa.  Huyu jamaa bwana ni bonge la design wa mavazi, nguo unazoona alizovaa Diamond na wakina Barnaba, Ommy Dimpozi na Amini huyu ndio aliyechora mpango mzima utakavyokuwa. Anaitwa Martin Kadinda  Anaitwa Esi yeye alikuwa akishughulika na usafi wa Diamond na kuonekana kwa steji kweli kamweka sawa raisi wa Wasafi DIAMONDS ARE FOREVER RED CARPET @Mlimani City Dar es Salaam Hapa ndipo palipokuwa sehemu ya wageni wote kupiga picha kabla yakuingia ukumbini, nimependa mwonekano ulivyokuwa umekaa, big up kwa waandaaji.    PICHA ZOTE NA STORY NI KUTOKA KWA DJCHOKA

TIMU YA PUBLIC RELATIONS (PR2) YATINGA ROBO FAINALI YA FAWASCO KWA KISHINDO

Image
Hatimaye leo katika kiwanja cha Nyegezi Seminary, timu ya PR2 imeweza kuonyesha uwezo wake wa kusakata soka baada ya kuichapa Timu ya Baso2 goli 1-0 na kuweza kuingia Robo fainali.Timu ya PR 2 imekuwa ikakabiliwa na mizegwe mbalimbali pindi wawapo viwanjani hasa pale wachezaji wake mahili wanapopigwa kadi Nyekundu na hivyo kukosa michezo muhimu kama wa leo.  "kila siku sisi tu kuonewa wachezaji wetu wamekuwa wakichezewa vibaya mara kwa mara lakini Refa anapeta tu”amekaliliwa mmoja wa mashabiki kutoka PR. Blog hii imeweza kufanya mahojiano na baadhi ya wachezaji wa timu ya PR kuwa safari hii wamejipanga sana kwa michezo yote iliyobaki na watajitahidi kadri ya uwezo wao na kuhakikisha kuwa safari ya kwenda Kagame ni ya kwao,na mamillion yote yanayotolewa na chuo cha Mt.Augustino katika mashindano haya ya FAWASCO yanabaki mikononi mwao. Angalia na video baada ya mechi pamoja na picha zilizochukuliwa baada ya ushindi…japokuwa hazikuwa katika ubora wa kutosha.

MIKAKATI YA KUWEKA MANISPAA YA MUSOMA SAFI YAZIDI KUBOREKA

Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara imejiwekea malengo ya kufanya usafi wa mazingira kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ili kuweka mji huo katika hali ya usafi. Akisoma Risala siku ya uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya usafi wa mazingira, Afisa Afya wa Manispaa hiyo, Peter Mtaki alisema kuwa uzinduzi huo utakuwa chachu uya uendeshaji wa usafi wa mazingira kwa kila mtu, kaya, nyumba, mtaa na kata. “Pia kampeni hii itafanya watu wabadili tabia na kuona kuwa suala la usafi si la watumishi wa Idara ya Afya pekee ni suala la mtambuka kila mtu kwenye eneo lake analoishi na anakofanyia kazi mazingira yake yawe safi,” alisema Mtaki. Alisema kuwa halmashauri hiyo lishatunga sheria ndogo ya usafi wa mazingira ambayo mpaka sasa ndiyo inayotumika ambapo sheria hii inamtaka kila mkazi kuweka eneo lake safi kuanzia majumban, eneo lake la kazi na maeneo ya biashara pamoja na kuchangia kiasi cha shilingi 500kama ada ya usafi. Vile vile halmashauri ilianza kuunda vikundi vya usafi katik

ZAMARAD AMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUJIFUNGUA SALAMA

Image
Mtangazaji wa Kipindi cha TAKE ONE cha Clouds TV, Zamaradi Mketema juzikati alijifungua mtoto wa kiume katika Hospitali ya Aga Khan na kumshukuru Mungu kwa kuutua mzigo huo salama. Akichonga na mpekuzi wetu  hivi karibuni jijini Dar, Zamaradi alisema kipindi chote cha ujauzito wake kuna waliodhani angejifungua kwa operesheni lakini Mungu amekuwa upande wake. “Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kuniwezesha kujifungua salama kwa njia ya kawaida. Nafurahi kumpata mtoto huyu wa kiume na huu ni mwanzo wa maisha mapya, ” alisema Zamaradi. Mtangazaji huyo amejifungua zikiwa zimebaki siku chache kwa wasanii wa filamu Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ na  Shamsa Ford nao wajifungue.

WANA MWANZA KAZI KWENU SASA

Image

DJ ZERO KUWAKILISHA USHINDANI KATI YA MA-DJ WA REDIO NA MA-DJ WA CLUB KATIKA USIKU WA REDDS LIPS CLUB MWANZA

Image

BAADA YA MGOMO HATIMAYE DALADALA ZAREJEA KUTOA HUDUMA.

Image
Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje akizungumza na madereva hao kuwasihi kurejea katika huduma kwani wananchi wanataabika. Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow akiwataka madereva hao kurudi katika huduma kwani suala lao tayari limekwishafika katika vyombo husika. Wakati huo huo Mwenyekiti wa chama cha madereva wa daladala Kanda ya Ziwa Protas Dede, amewaomba radhi wananchi kwa hali iliyotokeza na usumbufu walioupata kwani imewabidi kuchukuwa hatua hiyo kwa dhamira ya kutetea haki yao ili mambo yaende sawa. Dereva wa daladala akitoboa kero zake mbele ya wanausalama barabarani. Sasa ni zamu ya mwanausalama.. Mwisho ikawa ligi... Hivi ndivyo hali ilivyokuwa huku jeshi la polisi likiimarisha ulinzi eneo la kusanyiko viwanja vya Ghand Hall jijini Mwanza. Usalama uliimarishwa kama kawa.. Haikujulikana ni nini kilikuwa kimewasibu wanafunzi hawa hata wakafungwa pingu za kamba wakielekea kituo cha polisi kati.            picha na story nzima ni kutoka www.gsen

TWANGA PEPETA KUWAPA BURUDANI WAKAZI WA MUSOMA

Image
Bendi ya Muziki wa Dansi ya Twanga Pepeta imepania kukonga nyoyo za wapenzi wa bendi hiyo na wapenzi wote wa Muziki Mjini Musoma siku ya Ijumaa ya Machi 31 pale watakapofanya onyesho lao la kwanza Mjini hapa baada ya kufanya hivyo takribani miaka 3 iliyopita. Akizungumza na mwakilishi wa blog hii kutoka Musoma Bwana Shomari Binda kwa njia ya simu wakiwa njiani kuja Musoma,mratibu wa ziara hiyo ambayo ni maalumu kwa wakazi wa Kanda ya ziwa Martin Sospeter amesema kuwa wamefanya maandalizi ya kutosha kwa muda wote ili kuhakikisha wanatoa burudani ambayo itakidhi haja kwa wale wote watakaobahatika kufika kuangalia onyesho la bendi hiyo. Amesema katika ziara hiyo wataitambulisha Album yao mpya inayokwenda kwa jina la Dunia Daraja ambapo ndani yake kuna nyimbo kama vile Mapenzi hayana kiapo,Penzi la Shemeji,Mtoto wa Mwisho pamoja na nyi ngine zilizomo katika Album hiyo. Martini amesema kuwa licha ya kupata Burudani ya nyimbo mpya za Bendi hiyo,wapenzi wa Twanga Pepet

HUDUMA MPYA YA KISASA INAYOKUUNGANISHA MTANDAO WA MICHUZI BLOG BURE

Image
Tovuti yako uipendayo inakupa huduma ya kujivinjari bure kutoka Uhuruone Muhidini Issa Michuzi akishikiriana na Uhuruone wanawapatia wakazi wote wa Dar es Salaam huduma ya “Wifi hotspots” ambayo itawapa wakazi wote wa Dar es Salaam huduma ya bure ya kutembelea tovuti ya Michuzi. Kwa kupitia mitambo yao ya “Wifi Mesh” iliyopo Dar es Salaam ambayo imeunganishwa na tovuti ya Michuzi,wakazi wa Dar es Salaam wanatangaziwa kwamba wawashe kompyuta zao na kuunganishwa na taarifa za punde bila gharama yoyote. Akikaririwa katika mahojiano ndugu Issa Michuzi alisema hivi, “Ni mapinduzi ya kweli ambapo Watanzania wanachukua hatua katika kuleta taarifa mbalimbali kwa wananchi katika viwango nafuu. Ninaamini hii itaongeza mawasiliano kwa watu wetu na ni ndoto yangu kwamba tovuti ya Michuzi itakua huru kufika kwa Watanzania wote hivi karibuni”. Akiwa ofisini Bwana Rajabu Katunda alisema, “Uhuruone imejikita katika kutoa huduma kwa jamii na tumegundua

WABUNIFU WA MAVAZI NA WANAMITINDO KUIWAKILISHA TANZANIA KWENYE ONYESHO LA 'SOUTH AFRICA FASHION WEEK'

Image
Millen Magese (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanamitindo na wabunifu watakaokwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki katika maonyesho ya 'South Africa Fashion Week ' WABUNIFUwatatu, Doreen Estazia Noni anayetumia Lebo ya eskado bird , Jamila Vera Swai na Evelyne Rugemalira wamepata nafasi ya kuchaguliwa kwenda kwenye maonyesho ya mitindo yajulikanayo kama South Africa Fashion Week nchini Afrika kusini kupitia kampuni ya Millen Magese Group company Limited. Wabunifu hao watapanda jukwaani siku ya Aprili Mosi katika onyesho linalobeba jina la Tanzania International Fashion Exposé (TIFEX) by Millen Magese introducing Eskado Bird, Jamila Vera Swai and Evelyne Rugemalira. Millen alipata fursa ya kutembelea wabunifu hao na kujionea jinsi walivyokuwa wabunifu katika fani hiyo na kuhamasika kuwachukua na kushiriki katika maonyesho hayo maarufu ya mitindo katika bara la Afrika. Alisema kuwa amevutiwa sana na jinsi walivyokuwa

MANISPAA YA MUSOMA YAANDAA MIKAKATI YA KUBORESHA USAFI

Na Shomari Binda, Musoma Halimashauri ya Manispaa ya Musoma Mkoani Mara imeandaa mikakatia mbalimbali ya kuhakikisha Manispaa hiyo inakuwa katika hali ya usafi na kuwa miongoni mwa Miji misafi hapa Nchini kama ilivyokuwa katika Miaka ya nyuma. Kauli hiyo imetolewa jana na Afisa wa Afya wa Manispaa ya Musoma Peter Mtaki Ofisini kwake alipokuwa akizungumza na BINDA NEWS kuhusiana na maandalizi ya uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya Usafi wa mazingira itakayoanza Machi 30. Alisema moja ya mikakati ambayo wameipa kipaumbele ni pamoja na kusimamia Sheria ndogo ndogo za usafi wa Mazingira zilizotungwa mwaka 2010 ambazo bado zinaendelea kutumika hadi sasa lakini zimekuwa hazizingatiwi na Wananchi. Mtaki alidai Sheria hizo zinamtaka kila mkazi kuweka eneo lake safi kuanzia majumbani,eneo lake la kazi na maeneo ya Biashara pamoja na kuchangia gharama za Usafi kama ada ya Usafi. Alieleza kuwa Sheria hiyo inatamka kwa wale wanaokuwa wagumu wa kutojali usafi na ku