ZAMARAD AMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUJIFUNGUA SALAMA


Mtangazaji wa Kipindi cha TAKE ONE cha Clouds TV, Zamaradi Mketema juzikati alijifungua mtoto wa kiume katika Hospitali ya Aga Khan na kumshukuru Mungu kwa kuutua mzigo huo salama.

Akichonga na mpekuzi wetu  hivi karibuni jijini Dar, Zamaradi alisema kipindi chote cha ujauzito wake kuna waliodhani angejifungua kwa operesheni lakini Mungu amekuwa upande wake.

“Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kuniwezesha kujifungua salama kwa njia ya kawaida. Nafurahi kumpata mtoto huyu wa kiume na huu ni mwanzo wa maisha mapya,alisema Zamaradi.

Mtangazaji huyo amejifungua zikiwa zimebaki siku chache kwa wasanii wa filamu Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ na  Shamsa Ford nao wajifungue.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA