TIMU YA PUBLIC RELATIONS (PR2) YATINGA ROBO FAINALI YA FAWASCO KWA KISHINDO

Hatimaye leo katika kiwanja cha Nyegezi Seminary, timu ya PR2 imeweza kuonyesha uwezo wake wa kusakata soka baada ya kuichapa Timu ya Baso2 goli 1-0 na kuweza kuingia Robo fainali.Timu ya PR 2 imekuwa ikakabiliwa na mizegwe mbalimbali pindi wawapo viwanjani hasa pale wachezaji wake mahili wanapopigwa kadi Nyekundu na hivyo kukosa michezo muhimu kama wa leo. 

"kila siku sisi tu kuonewa wachezaji wetu wamekuwa wakichezewa vibaya mara kwa mara lakini Refa anapeta tu”amekaliliwa mmoja wa mashabiki kutoka PR. Blog hii imeweza kufanya mahojiano na baadhi ya wachezaji wa timu ya PR kuwa safari hii wamejipanga sana kwa michezo yote iliyobaki na watajitahidi kadri ya uwezo wao na kuhakikisha kuwa safari ya kwenda Kagame ni ya kwao,na mamillion yote yanayotolewa na chuo cha Mt.Augustino katika mashindano haya ya FAWASCO yanabaki mikononi mwao.

Angalia na video baada ya mechi pamoja na picha zilizochukuliwa baada ya ushindi…japokuwa hazikuwa katika ubora wa kutosha.
















Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA