TUSIWAUMIZE WENZETU KWA KUWAVISHA PETE ZA UCHUMBA
Siku mbili zilizopita nilipata message kutoka kwa rafiki yangu ambaye ni msichana...kiukweli nilipatwa na kigugumizi cha mikono ni kwa jinsi gani nitaweza kumshauri kwa kupitia ujumbe mfupi wa mkononi yaani sms aweze kuona kwamba swala lililomtokea ni la kawaida kwa maana kwamba binadamu tumeumbiwa matatizo na ni jukumu letu kupambana nayo mpaka kupata suluhisho la matatizo hayo. Story ilikuwa hivi,dada huyu ambaye ndio rafiki yangu alinitumia message akiniambia kuwa miezi 2 iliyopita amevalishwa pete ya ndoa na mchumba wake, sasa cha kushangaza ni kwamba wamekuwa katika mahusiano na mchumba wake huyo kwa muda wa miaka 2 bila binti kujua lolote kuwa mchumba wake alishazaa na mwanamke mwingine japokuwa binti alisha muuliza mchumba wake huyo kama ana mtoto lakini jamaa alikuwa akipinga vikali kuwa hajawai na wala hana hata wa kusingiziwa, jibu ambalo lilikuwa lkimfurahisha dada huyu na pia kuambiwa kuwa yuko peke yake hana mahusiano mengine ya nje. Utamu wenyewe wa stor