MADIWANI CHADEMA WAGOMEA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI TARIME


NA SHOMARI BINDA KUTOKA MUSOMA



MADIWANI 16 wanaotokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamegomea kuingia katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo kwa ajili ya kushiriki kikao maalum cha Baraza la madiwani kwa ajili ya kumchagua makamu mwenyekiti kwa kile kilichoelezwa kupata maelekezo ya kugomea kutoka kwa viobgozi wa kitaifa wa Chama hicho.


Akitoa maelezo kabla ya kufunguliwa kwa kikao hicho,Mkurugenzi wa Halimashauri hiyo Athman Akalama alisema amesikitishwa na kitendo cha madiwani hao kugomea kikao hicho kwa kuwa walikuwa na taarifa ya wiki moja lakini ghafla walikigome mapema kabla ya kuanza kwa kikao.


Alisema kutokana na muongozo wa Tamisemi juu ya mabadiliko na uundwaji wa Halimashauri mbili katika Wilaya hiyo ili lazimika kufanyika mchakato wa kuandaa muongozo wa namna ya kuunda Halimashauri hizo na madiwani wa vyama vyote walishirikishwa tangu hatua ya kwanza.


Akalama alisema mabadiliko hayo kutoka Tamisemi kuingiza Mamlaka ya Mji katika Halimashauri na kuundwa kwa Halimashauri mbili yan alengo la kuleta Maendeleo kwa Wananchi wa Wilaya ya Tarime na hoja ambazo anadai zimetolewa na mwishoni na madiwani wa Chadema ni kutaka kukwamisha Maendeleo.


Alisema hoja ambazo zimetolewa na madiwani hao ni kutaka kupata orodha ya wajumbe wa Halimashauri ya Mji wa Tarime pamoja na ukomo wa kamati zitakazoundwa baada ya uchaguzi zikiwa katika maandishi hali ambayo hakuweza kuitekeleza kutokana na kuitaka kwa uharaka.


Mkurugenzi huyo wa Halimashauri ya Wilaya ya Tarime alisema madiwani hao hawakuleta maombi ya hoja zao katika maandishi kama walivyoomba licha ya kuwa na muda wa kutosha na walimpelekea barua ya uteuzi wa jina la mgombea wa nafasi ya makamu mwenyekiti tangu machi 18.


“Kwa kweli mimi nashangaa uamuzi wa madiwani kutoka Chadema kugomea kikao hiki maana nimekaa nao kwa muda wa kutosha na kupeana nao ushauri na maelekezo kuhusu jambo hili lakini ghafla wamegomea,lakini kutoka na unyeti wa suala hili nawaomba waheshimiwa madiwani mnipe muda wa kwenda kuwasikiliza tana ila kwa muda mfupi ntaitisha Baraza tena,’’alisema Akalama.


Baada ya Mkurugenzi kutoa maelezo hayo madiwa waliokuwa katika ukumbi huo kutoka CCM na CUF walitaka kuendelea kwa kikao hicho na kufanyika  kwa uchaguzi wa makamu mwenyekiti kwa kile walichodai kuhailisha kikao hicho ni kufanya matumizi mabaya ya fedha za Wananchi kwani ni ghalama kubwa kuandaa Baraza.


Kutokana na hoja za madiwani wa vyama hivyo hatimaye uchaguzi wa kumpata makamu mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Tarime ambaye ataongoza kamati mbili ambazo ziliundwa kwa ajili ya ugawaji mali katika Halimashauri mbili za Wilaya ya Tarime ulifanywa na madiwani 24 wakiwemo 23 kutoka CCM na 1 kutoka CUF ambapo Diwani wa Kata ya Kitare Daud Wangwe (CCM) alishinda kwa kupata kura 23 dhidi ya kura moja ya Diwani aliyekuwa amepitishwa na Chadema Charles Ndesi.       


Akizungumza na MTANZANIA,Diwani wa kata ya Sababa Christopher Chomete (Chadema) ambaye alichaguliwa kuwa mmoja wa wanakamati watakaohusika katika ugawaji wa mali alisema hautambui uchaguzi huo kwa kuwa haukufuata utaratibu na hawezi kukubali kuwa katika kamati hiyo.


Alisema taratibu ambazo zimevunjwa ni pamoja na kutokuzingatia kanuni za kuendesha baraza kwa kuwa theruthi mbili za wajumbe waliotakiwa kushiriki  kikao hicho hazikutimia bali waliendesha kikao hicho kwa kuitimia shinikizo la madiwani wa CCM.

Chomete alisema kutokana na kikao hicho kutokuwa halali hawezi kukubali nafasi ya uteuzi wa mjumbe wa kamati kutoka Halimashauri ya Mji wa Tarime na madiwani wote wanaotokana na Chadema hawataweza kuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya Baraza la madiwani kama hawatabatilisha kikao walichopfanya cha kumchagua makamu mwyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Tarime

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA