WAMILIKI WA VIWANDA NA HOTEL JIJINI MWANZA WATAKIWA KUFANYA UKAGUZI WA MAZINGIRA
Uongozi wa Hotel ya Malaika beach Resort, umetakiwa kufanya ukaguzi wa mazingira katika eneo la hotel hiyo na kuto repoti ili kuweza kuhepaukana na uharifu wa mazingira utiririshaji wa maji taka,katika ziwa Victoria.
Hayo yameelewa leo na Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais mh. Charles Kitwanga alipotembelea baadhi ya hotel na viwanda vilivyopo katika wilaya ya Ilemela jijini Mwanza, ili kujione hali halisi ya utunzani wa mazingira.
Alipotembelea kiwanda cha Nondo cha Nyakato steel, Mh. Kitwana aliwaasa wamiliki wa kiwanda hicho kutumia njia za kisasa za kuweza kuhepuka kutoa moshi mzito ambao umekuwa ukilalamikiwa na wakazi wa maeno hayo kuwa nyakati za usiku moshi huo huaribu mandhari na hali ya hewa na kuhatarisha afya za wakazi wa karibu na eneo hilo.
Aidha wamiliki wa kiwanda hicho pia wameshauriwa,kuwajali wafanyakazi wao kwa kuwapatia vifaa vya usalama kazini ikiwa ni gloves pamoja na mabuti kutokana mazingira wanayofanyia kazi na kutokuziweka afya zao katika mazingira hatarishi.
Alipotembelea kiwanda cha nguo cha Mwanza MWATEX, Mh. Naibu Waziri hakuridhiswa sana na mfumo wa kiwanda hicho wa utoaji wa maji taka na kuwashauri wamiliki wa kiwanda hicho kufanya tena ukaguzi wa mazingira na kurekebisha upya njia za kiwanda hicho za utoaji wa maji taka.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi Amina Masenza ameeleza kuwa katika suala zima la utunzaji wa mazingira wilaya yake inakumbana na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya kitaala vya kufanyia tathimni ya athari za mazingira katika sehemu za kazi na kuongeza kwa gharama za kufanya uchunguzi wa sampuli za maji taka zitokazo viwandani ziko juu.
source: fullshangweblog
Comments
Post a Comment