Waangalizi wa Kanda Uchaguzi Kenya Wasifia Zoezi Zima


Kinana addresses press on preliminary repoprt 5 March 2013
Na Isaac Mwangi, EANA-Arusha
WAANGALIZI wa Kanda katika uchaguzi mkuu wa Kenya wameonyesha kuukubali mwenendo wa upigaji kura Jumatatu kuwa ulikwenda sawia na kutaka hali hiyo iendelee katika hatua nyingine zilizobaki za uchaguzi huo.
Taarifa hiyo imetolewa na Timu ya Pamoja ya Waangalizi wa Kanda kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Soko la Pamoja la Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) na Mamlaka ya Maendeleo Afrika (IGAD), Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA) limeripoti.
“Ingawa kulikuwepo na changamoto kadhaa kuhusu uhakiki wa wapiga kura, timu hiyo imehitimisha kwamba uchaguzi mkuu wa 2013 umefikia viwango vya kanda, bara na vya kimataifa kuwa ni wa kuaminika na uwazi,” ilieleza taarifa iliyotolewa Jumanne.
Taarifa ya awali ya waangalizi imetathmini hali ya kisiasa kuelekea kwenye uchaguzi,uteuzi wa wagombea uliofanywa na vyama vya siasa, kampeni na nafasi ya wapiga kura na vyombo vya habari kwenye mchakato mzima wa uchaguzi huo.
Timu hiyo katika taarifa yake imeleza pia kwamba ilitathmini siku ya upigaji kura yenyewe ikiwa ni pamoja na idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura,mwenendo wa upigaji kura,wasimamizi,masuala ya usalama,waangalizi na mawakala wa vyama vya siasa.
Taarifa hiyo ya Timu, iliipongeza Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa kusimamia uchaguzi huo kwa weledi, pia iliwapongeza maafisa usalama kwa kuhakikisha kwamba sheria na taratibu zinafuatwa katika kipindi chote cha mchakato wa upigaji kura.
“Matukio machache ya ghasia hayakuweza kufunika mwendendo mzima wa amani katika uchaguzi huo,” taarifa ilisisitiza.
Taarifa hiyo ya waangalizi pia iliguswa na idadi kubwa ya kura zilizoharibika ambazo zinaweza kuleta athari katika matokeo. Ilisema hiyo inawezekana imetokana na wapiga kura kutoelewa sawia taratibu za upigaji kura. Taarifa hiyo ilisomwa na Kiongozi wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi ya Kanda, Abdulrahman Kinana aliyefuatana na viongozi wenzake wa timu za waangalizi za COMESA, EAC na IGAD.
Kinana ambaye ni Spika wa zamani wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) alitoa wito kwa wagombea kuyakubali matokeo ya uchaguzi huo au kama wana malalamiko watumie njia inayokubalika ya kuyafikisha mahakamani. Makundi hayo matatu ya kanda yalikuwa na jumla ya waangalizi 78 waliosambazwa katika kaunti 40 kati ya 47 zilizopo nchini Kenya.

Comments

  1. If there is a change in the search engine algorithms, it is
    also up to the service provider to keep a watch on such activities.
    The objective is to arrange your passions as carefully as possible with your online promotion company.
    Users normally tend to visit websites that are at the top of
    this list as they perceive those to be more relevant to the query.
    SEO (search engine optimization) and keyword density are
    terms that scare many a writer who want to write for the internet.

    Thus, in minimum cost, you get an opportunity to increase your site ranking on Search Engine Result Page (SERP).
    It would cut the marketing project to fit it into your
    budget. Some SEO firms focus on content spinning and submitting articles.
    Relevant keywords ought to be used in the alt tags. Make buying easy for the
    customer and they will return often. What are the advantages of article submission.
    Search engine optimization is necessary for online businesses because it
    lets your website get found. For instance, how many TV viewers
    then came to your car lot and purchased a vehicle. Moving your
    hosting to a nearby country such as Canada or an offshore
    Caribbean host may provide the same latency times, but reduce the risk of having your website brought down
    by a mistake. Regardless of whether you like it, love it, or hate it,
    social media has become a major player in the SEO
    world, and it is a costly mistake to ignore it. This is where
    your innovative SEO marketing techniques can achieve a high search
    ranking for your budget motel whenever a user is specifically searching for a
    motel at your location. G) SEO basics -Image 6:
    Open Google. Online Advertising and SEO Marketing.

    A person can find all sorts of products available at various prices on
    the internet. They are looking up the the keywords you did research on to find what they are looking for.
    If customers like what they see, they just might
    go on reading.

    My homepage ... Home Page

    ReplyDelete
  2. I liκе the hеlρful info уou provide in your articles.
    Ι'll bookmark your weblog and check again here frequently. I'm quіte сertain I ωill lеarn many new stuff гight hеre!
    Good luck for the next!

    Hегe is my blog :: listwy styropianowe

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA