SOMA HOTUBA YA RAIS WA SAUTSO MH.MALISA ALIYOITOA WAKATI WA KUVUNJA BUNGE NA SERIKALI YA WANAFUNZI
President Office, C/o St. Augustine University of Tanzania
(SAUT), P.O. Box 307,
Malimbe Campus,
Nyegezi – Mwanza Region
WEBSITE:
www.sautsolink.blogspot.com
HOTUBA YA RAIS WA SAUTSO 2012/13 ALIYOITOA WAKATI WA
KUVUNJA BUNGE NA SERIKALI YA WANAFUNZI TAR.16/03/2013.
Mhe.Spika,
Mlezi
wa wanafunzi,
Makamu
Mkuu wa chuo Fedha na Utawala,
Mawaziri
na wabunge, Itifaki imezingatiwa.
Awali
ya yote natoa shukrani za dhati kwa wanafunzi, wafanyakazi na utawala wa Chuo
hiki kwa ushirikiano mkubwa mlionipatia kwa kipindi changu cha mwaka mmoja wa
uongozi. Nimejifunza mengi ndani na nje ya nchi. Hakuna uongozi usio na
changamoto lakini ukimtumainia Mungu atakushindia yote.
Pili
nilishukuru bunge lako tukufu, mawaziri
na viongozi kutoka utawala, waandishi wa habari na wadau wengine kwa kujitokeza kwa wingi kuja kunisikiliza
nikihutubia Bunge kwa mara ya mwisho kabla sijalivuja rasmi, kama nilivyopewa
mamlaka hiyo na Katiba ya SAUTSO Ibara ya 9.3.3 na Ibara ya 9.6.6 kwa pamoja.
Mhe.Spika,
Serikali
ya wanafuzi katika chuo kikuu cha Mt.Augustino 2012/2013 ilichaguliwa
ta.25/04/2012 kwa ushindi wa 70.1% dhidi ya 29.9% alizopata mpinzani wetu katika
uchaguzi uliofanyika kwa amani na utulivu lakini uliogubikwa na changamoto
nyingi. Huu ulikuwa ni ushindi mkubwa kuwahi kutokea katika historia ya
uchaguzi ya chuo hiki. Ushindi huu ulitoa tafsiri ya Imani kubwa ya wanafunzi
wa SAUT kwetu na kukubalika kwa sera zetu kwao kupitia Ilani yetu ya uchaguzi.
Mhe.Spika,
Wakati
tunaomba ridhaa ya kuongoza Jumuiya ya wanafunzi wa chuo hiki tulikuwa na Ilani
ya uchaguzi yenye vipaumbele 11. Tuna furahi kuwa muda wetu wa kuwepo
madarakani umekwisha nasi tunajivunia mafanikio ya 90% katika utekelezaji wa
Ilani yetu ya uchaguzi. Hiyo ni level ya juu sana ktk political achievement.
Mhe.Spika,
Vipaumbele
tulivyoainisha kwenye Ilani yetu japo kwa kuvitaja ni kama ifuatavyo. Kwanza ni
kuhakikisha miundombinu ya kujisoea nje ya madarasa inaboreshwa, Kupata ofisi
mpya ya SAUTSO, Kuimarisha Ulinzi na Usalama kwa wanachuo wote hasa wanaoishi
Off-Campus, Kuboresha miundombinu ya kujisomea madarasani kama Projectors na
Sound System, Kuhakikisha umeme wa uhakika kwenye maktaba ya chuo, Kuzuia
mfumuko wa bei za vyakula chuoni, Kuboresha sekta ya michezo, Kuhakikisha
gharama za bei za hostel za nje zinapungua, kuboresha sekta ya Afya na mwisho
ni kufanikisha ununuzi wa basi la chuo.
Mhe.Spika,
Tumefanikiwa
kurekebisha sound system za madarasani na projectors. naamini mmejionea wenyewe
kazi iliyofanyika na hakuna darasa linasumbua.
Tuliahidi
umeme wa uhakika Library, na nimepambana sana kwny vikao vya maamuzi ndani ya
chuo ikiwemo,
- University senate
- University management Board, kupeleka hoja ya kuhakikisha inatengwa bajeti ya kutekeleza hilo. Jitihada hizo zikazaa matunda na tayari zimenunuliwa solar panels zaidi ya 70 na zimeanza kufungwa ili library iwe na reliable source of energy. Nafarijika kwamba sasa wanafunzi wakiwa Library umeme ukakatika hawatafukuzwa tena kama ilivyokuwa awali.
Mhe.Spika,
Tuliomba
Serikali ya wanafunzi (SAUTSO) kupata ofisi mpya baada ya ofisi inayotumika
sasa kutokukidhi mahitaji ya shughuli za serikali za siku kwa siku. Nafurahi
kulijulisha bunge lako tukufu na umma wa SAUT kwa ujumla kuwa tumepata ofisi mpya opposite na Mwanjonde Lecture Theatre.
Tayari
tumeikarabati kwa kuboresha system ya choo, kuweka milango, na kuvunja baadhi
ya kuta ili ionekane ofisi badala ya nyumba ya kuishi. Tumeweka mashelf. Kwa
kifupi ukarabati ndani umemalizika hadi rangi, bado nje.
Japokuwa
ofisi imeshindwa kukamilika kwenye uongozi wetu lakini nafarijika kuwa serikali ijayo
itakuwa na ofisi mpya ambayo ni matunda ya juhudi zetu. Ofisi hii ina
vyumba 6 na ile ya zamani ina vyumba 3, hivyo kwa ujumla SAUTSO itakuwa na
vyumba 9 vya ofisi na kuwa Serikali pekee ya wanafunzi yenye ofisi
nyingi zaidi Tanzania.
Mhe.Spika,
Tuliahidi
kuboresha mazingira ya kusomea nje ya madarasa. Tulijitahidi kutafuta ufadhili
ndani na nje ya chuo na hatimaye tukafanikiwa kukutana na shirika maendeleo la
ujerumani ambao wameingia ubia (patnership na TiGo) katika kutusaidia.
As the result wamekubali kutujengea vimbweta
vya kusomea vya kisasa na kuboresha vilivyopo, kuanzia eneo la ATM hadi karibu madarasa
ya M10 na M9. Huu ni ufadhili mkubwa maana mradi huu utagharimu jumla ya sh. Mil.79.
Tayari mradi umepata baraka za Makamu Mkuu wa chuo fedha na utawala ambaye ameshasaini
mkataba wa kuwaruhusu kuanza kazi.
Pamoja
na pongezi kubwa tulizozipata kwa Vice Chancelor kutokana na jitihada zetu, tunaiasa
serikali ijayo itoe ushirikiano wa kutosha kuhakikisha mradi huu unaanza
kutekelezwa. kumbukeni mkilalala wanaweza kuona hamna nia hivyo hivyo
wakakata tamaa.
Mhe.Spika,
Tumepigania
wanafunzi 16 waliofukuzwa chuo kurudishwa masomoni baada ya kutetea rufaa zao
kwenye Board of Appeal. Mmojawapo ni mwenyekiti mstaafu wa chama cha wanafunzi
wanaosoma Kiswahili (CHAWAKAMA).Pia tulijitahidi kuwaombea msamaha wanafunzi
zaidi ya 260 wa Public Relations ambao management ilishauri wafukuzwe kutokana
na kufanya fujo kwenye chumba cha mtihani. We pled for clemency na wote
wakasamehewa.
Mhe.Spika,
Tuliahidi
kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali ya wanafunzi (SAUTSO) kwa kupunguza
matumizi yasiyo ya lazima. Na tumefanikiwa kupunguza matumizi ya SAUTSO kutoka
mil.240 za serikali iliyopita kufikia mil.136 kwa serikali yetu. Nilishukuru
bunge lako kwa kukubali mabadiliko hayo na kuipitisha bajeti yetu kwa 99% ya
kura zote zilizopigwa.
Mhe.Spika,
Tumeratibu
kwa ufanisi safari ya Rwanda kwa washindi wa Fawasco mwaka jana. Pia
tulifanikiwa kupeleka timu nne (4) kwenye SUSAUT Gathering ya Morogoro. Awali zilikuwa
zikienda timu (2) tu, yaani football na netball. Lakini chini ya uongozi wetu
tumefanikiwa kuongeza timu ya Basketball ambayo ilichukua ubingwa kwa kuvifunga
vyuo vingine zaidi ya 10 vilivyoshiriki. Timu yetu ya Basket ndio timu pekee
ambayo haikuwahi kupoteza mchezo wowote tangu mwanzo hadi mwisho wa mashindano.
Laiti tusingeipeleka ushindi huo tusingeupata.
Pia timu ya Volleyball ambao nao tuliwapeleka
wakashiriki kwa mara ya kwanza, waliingia fainali na kuibuka washindi wa pili.
Mhe.Spika,
Tumeandaa
makongamano, semina, na midahalo mbalimbali yenye manufaa kwa wanachuo kama
ifuatavyo:
-Kongamano katiba ambapo tulimwalika Deus
Kibamba (m/kiti Jukwaa la Katiba), Bw.Jimmy Luhende mkurugenzi wa asasi ya ADLG
na wageni wengine (08/12/2012).
-Kongamano la kujadili maadili ya taaluma ya
ualimu ambapo tulikuwa na Rais wa chama cha waalimu Adrian Mkoba (05/01/2013).
-forum
ya siku ya siku ya wanawake duniani ambapo tulimwalika Prof.Anne Tibaijuka
lakini kwa bahati mbaya akashindwa kufika (23/02/2013).
-Na wakati wa kuvunja bunge jumamosi ya tarehe
16/03/2013 tulihitimisha na forum ya uchumi ambapo tulikuwa na Mh.Tundu Lissu
na mkurugenzi wa TPDC Bw, Yona Killagane aliyekuja kwa niaba ya waziri wa
nishati na madini Prof.Sospeter Muhongo.
Forum zote hizi zimesaidia sana kuongeza upeo
wa wanafunzi wetu ktk mambo mbalimbali na kupata fursa ya kuuliza yale
yaliyokuwa yakiwatatiza.
Mhe.Spika,
Tumefanikiwa
kuboresha mashindano ya FAWASCO kwa kutafuta udhamini NMB na TiGo.
NMB wametoa jezi, mipira, usafiri wa timu
kwenda kambini. In advance pia watatoa flat screen mbili za inch 52 kwa SAUTSO
ijayo. Tayari tumeshasign mkataba ndio maana uwanja wa Raila Odinga unashine
kwa flies za NMB.
Hizo
ni juhudi zetu kama Serikali yetu inayoondoka madarakani. Awali mimi na wizara
yangu ya michezo tulikutana na Mkurugenz wa NMB Lake zone Mr.Straton Chilongola
na baadae tukakutana na Mkurugenzi wa Masoko NMB taifa Mr.Imani Kajula katika
kutekeleza azma hiyo.
In
return NMB tumekubali wafungue ATM yao hapa chuoni ili kutengeneza two ways symmetrical
communications kati yao na jumuiya ya chuo hiki kupitia Corporate Social Responsibility.
Natumaini mmeiona ATM hiyo na kwa wateja wa NMB anzeni kuitumia kwa ari, nguvu
na kasi zaidi.
Mhe.Spika,
Tunafarijika kuona ATM ya NMB iliyotokana na
juhudi zetu, lakini tunafarijika zaidi kuona wachezaji wetu wakiwa wanapendeza
kwny jezi za NMB.
Kwa
upande wao TiGo wao watachangia Mil.6 kufanikisha Fawasco ya mwaka huu na
tayari wamekabidhi kwa utawala (mbele ya DVCAF) vifaa vyenye thamani ya
mil.3.5. Tigo pia watafanya tamasha kubwa siku ya fainali ambapo wamedai
kumleta msanii wa kimataifa (watamtaja badae)
Mhe.Spika,
Kwa ujumla ufadhili wa Tigo na NMB
utakagharimu takribani mil.15. Haya ni mafanikio makubwa sana kwetu, kwa
management na kwa wanafunzi wote kwa ujumla. Hakuna serikali iliyowahi kufanya
hivi. Wakati wengine walikuwa wanaomba fedha management, sisi tumetafuta fedha
kwa asasi za nje na kuzileta management. Hizi juhudi zinazopaswa kupongezwa na
kila mpenda maendeleo.
Mhe.Spika,
Tumehakikisha
fedha za meals & Accommodation zinafika kwa wakati, (unless kwa wale
wachache waliokuwa na special case). Pia hii ni serikali pekee ambayo
imehakikisha fedha za Research zinafika kwa muda muafaka (kabla wanafunzi
hawajafanya mitihani yao ya mwisho).
Mhe.Spika,
Tuliahidi
bei ya chakula itabaki kuwa 1200 kwa 1500 na tumehakikisha hilo limetekelezwa.
Kuna kipindi wazabuni walipandisha bei kinyemela kufikia sh.2000 kinyume na
mikataba yao ya zabuni kwa kulalamikia cost of production. Lakini tuliunda
kamati maalum iliyofanya uchunguzi wa kina juu ya madai hayo na kubaini kuwa
madai hayo hayakuwa na ukweli wowote.
Hivyo tukalazimika kutoa notice ya saa 24 kwa
wazabuni kurudisha bei ya kawaida .(1200 kwa 1500). Tunawashukuru kwa kutii
agizo hilo na kurudisha bei ya kawaida kama ilivyoelekezwa ktk mikataba yao.
Yamkini tuliibua migogoro na baadhi ya wazabuni (hatuna budi kuomba radhi) lkn
nia yetu ilikuwa kulinda haki za waliotuchagua.
Mh.Spika,
Tuliahidi
pia kuwa na nembo (logo) yetu kama serikali ya wanafunzi badala ya kutegemea
logo ya utawala ili kuweza kuwa na corporate identity yetu. Nafurahi
kulijulisha bunge lako tukufu kuwa tumefanikiwa kutengeneza logo ya SAUTSO tangu
mwezi August mwaka jana (2012) baada ya nembo hiyo kudhbitishwa na utawala.
Mhe.Spika,
Nembo
hii sio tu kuwa itatumika katika shughuli mbalimbali za serikali ya wanafunzi,
bali itabaki kuwa alama ya kumbukumbu kwa serikali yoyote itakangoza SAUTSO
baada yetu, hatakama ni baada ya miaka elfu moja. Pongezi kwa wizara ya Habari
na mawasiliano kwa juhudi kubwa walizozifanya kufanikisha swala hili.
Mhe.Spika,
Kwa
kifupi tumefanya mengi sana, japo hatuwezi kueleza kila moja lakini tumejitahidi
kadri ya uwezo wetu kutimiza yale tuliyoahidi. Kama kuna ambayo tumeacha
tunaamini watakaokuja nao watafanya kwa nafasi yao.
Mhe.Spika,
Nitumie
pia fursa hii kuipongeza Tume ya uchaguzi iliyoundwa jumamosi na kuapishwa juzi
na mwanasheria mkuu wa chuo. Nimpongeze Mh.Lumuli Makala kwa kuchaguliwa M/kiti
wa Tume. Naamini yeye na jahazi lake wataongoza tume ktk kufanya uchaguzi huru
na haki na kumpata Rais ambaye ni chaguo la wana-SAUT.
Nitoe
shukrani za pekee kwa baraza langu la mawaziri ambalo kila mmoja amepigana
kiume kuhakikisha anawatumikia kwa ufanisi watu wa SAUT.
Nimshukuru
Makamu wangu Consolatha Michael, Waziri Mkuu Baraka Mnkeni na Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais Nice Mberesero kwa kunishauri kwa busara ktk kipindi chote cha uongozi
wangu.
Mhe.Spika,
Nikushukuru
pia wewe Spika wa Bunge la SAUTSO (Mh.Lutehanga Eric) kwa kuongoza bunge kwa
hekima na kuhakikisha bunge linatimiza kazi yake ya kuisimamia serikali.
Zaidi
ya yote nimshukuru Makamu Mkuu wa chuo Rev.Dr.Charles Kitima kwa ushirikiano
mkubwa kwa SAUTSO. Kila ninapomuona naona matumaini hata kama kuna kiza mbele
yangu. Nimshukuru pia kwa kutusaidia kufanikisha safari ya SAUTSO Zambia,
Malawi Rwanda na kwingineko. Mungu ambariki sana na ampe maisha marefu na yenye
Baraka.
Mhe.Spika,
Niushukuru
uongozi wote wa chuo kwa ujumla wake, kwa kuanzia na Makamu Mkuu wa Chuo
Taaluma, Makamu Mkuu wa Chuo Fedha na Utawala, Mwanasheria Mkuu wa Chuo na Mlezi
wa Wanafunzi (Dean of students) kwa kutusaidia kila tulipokwama. Hawakuchoka
tulipohitaji msaada wao. Tunashauri serikali ijayo iwatumie kwa ufanisi maana
ni hazina ya maarifa na hekima.
Mhe.Spika,
Kwa
moyo wa dhati niwashukuru waalimu wangu walioniwezesha kufika hapa, na hata
nilipokuwa kiongozi hawakuniacha bali walizidi kunishika mkono na kuniongoza
pale nilipoteleza. Nimshukuru kipekee Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Umma
Madam Duwe kwa kunishauri, kunionya na kunielekeza bila kuchoka.
Nitakuwa mchoyo wa fadhila bila kuwashukuru
wanadarasa wenzangu wa B.A in Mass communications (mwaka wa tatu) kwa
ushirikiano mkubwa walioonesha tangu wakati wa kampeni hadi sasa. Hawakuchoka
kunishauri, kunionya nilipokosea, kunielekeza. Hata nilipozidiwa na majukumu na
kushindwa kufika darasani bado walijitoa kunisaidia. Pia shukrani hizi ziwafikie wanafunzi wote wa
SAUT.
Wa
mwisho japo ni wa kwanza kwa umuhimu ni wazazi wangu Mr&Mrs Malisa Joseph
Elisante.
Mhe.Spika,
Zaidi
ya wote nimshukuru Mwenyezi Mungu wa mbinguni kuniumba na kuwa nami ktk kila hatua
ya maisha yangu,
Leo mimi ni Kiongozi wa SAUTSO, kiongozi wa
shirikisho la vyuo vikuu vya SAUT na kiongozi wa shirikisho la wanafunzi vyuo
vikuu Afrika Mashariki (EACSU) kwa uweza wako Mungu. Wewe ndiwe ujuaje nitokako
na ninakoelekea, uniongoze kuzifikia ndoto zangu. Wewe husema iwe ikawa, sifa
na utukufu vikurudie (Zaburi 8:1-8).
WITO KWA SERIKALI IJAYO.
Uongozi ni kujitoa sadaka, uongozi ni
kujinyima, Uongozi wa kweli ni mzigo. Kuna wakati utalazimika kuacha jambo hata
kama unalipenda kwa sababu wewe ni kiongozi, na kuna wakati utalazimika kufanya
jambo hata kama hupendi ili kuwatumikia watu.
Ukiwa
kiongozi utapoteza masomo, utakosa muda wa kufanya mambo yako binafsi, utakosa
quiz, assignment kwa ajili ya kuwatumikia watu. GPA yako itatetereka kwa ajili
ya utumishi uliotukuka. Kuna wakati utatumia hadi fedha zako binafsi ili mambo
yasikwame, kuna wakati utakosa hata muda wa kula, muda wa kulala, pengine hata
muda wa kujisomea lakini ni wachache sana watakaoappreciate juhudi zako.
Usife
moyo, usikate tamaa, songa mbele ukimwomba Mungu. Wapo watakaokudisappoint kwa
kukosa fursa may be ya uwaziri na kudiscredit kila unalofanya lakini usikate
tamaa.
Unaweza
kukosa muda wa kufanya jambo lolote binafsi. Muda wa kula, muda wa kuwajulia
hali ndugu zako (wengine kwa kutokujua watasema unaringa baada ya kuwa
kiongozi), unaweza kukosa hata muda wa kulala, lakini jitahidi usikose muda wa
kufanya mambo mawili makubwa:Muda wa kusali na Muda wa kufanya kilichokuleta
chuoni (kusoma). Hata kama utapata muda kidogo, utumie vizuri.
Mhe.Spika,
Baada
ya kusema hayo natangaza kuwa kwa mamlaka niliyopewa na Katiba ya SAUTSO
nimelivunja rasmi bunge la serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Mt.Augustino
mwaka 2012/2013, tayari kwa mchakato wa uchaguzi.
NAWATAKIA UCHAGUZI HURU, HAKI NA
WENYE AMANI. MUNGU AWABARIKI WOTE.
Malisa
Godlisten
Rais
SAUTSO 2012/2013.
Comments
Post a Comment