BAJAJI YA MIZIGO YAPATA AJALI KWENYE TRAFIC LIGHT JIJINI MWANZA

Ni bajaji ya mizigo ambayoilikuwa na mizigo ya mafuta ya kula, chumvi, sabuni pamoja na unga imekula mzinga ikiovateki roli na kukuta roli upande wa pili limepaki na dreva wa bajaji alipojaribu kurejea kwenye upande wake wakushoto ndipo brekizikamzidia akajibamiza nyuma ya roli alilokuwa akiliovateki.
Wananchi waliofurika eneo la tukio

Bahari ya mafuta ya kula....
Dereva wa bajaji hii alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando kupatiwa matibabu mara baaada ya kupata majeraha makubwa ya kutisha huku akimuacha mwenye mali ambaye alikuwa amepakizwa nyuma na mizigo akiwa amelowa mafuta na akiwa hana hata jeraha moja.
Taswira amili na wananchi mashuhuda.
Hii ndiyo mizigo iliyosalimika wakati ile ya mafuta yooooote yakimwagika kupitia ajali hiyo.
Ni hasara ingawa kunausalama kiasi.
Askari wa jeshi la polisi Mwanza wakipima ajali hiyo. 

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA