VIDEO:ULIMISS KUANGALIA COKE STUDIO WAKATI DIAMOND AKIPERFORM?ANGALIA HAPA

Naseeb Abdul aka  diamond platnumz ni msanii anayetishakatika ukanda wa Afrika Mashariki katika miondoko ya  bongoflava kwa sasa.tokea atoke na ngoma yake ya kamwambie Naseeb hajawai kuzimika katika ulimwengu wa muziki wa bongo. Diamond ni moja ya wasanii anayejituma sana katika muziki huu wa bongo fleva na kila kukicha amekuwa ni mbunifu wa kuongeza thamani kwa kile anachokifanya,akiwa na zaidi ya nyimbo 130 kwenye library yake,week iliyopita alionekana ndani ya Coke studio na kuirudia ngoma ya temptation na msanii HHP kutoka Afrika ya kusini,hii imemfanya diamond kubadilika kimziki na kuonyesha style nyingine ambayo imemfit pia.
Akiwa na umri wa miaka 24 tu kwa sasa , Diamond alianza muziki tokea akiwa na miaka 13 na alikua akicopy baadhi ya miziki na baadae baada ya kujiunga na sekondari mama yake mzazi alimwambia aachane na muziki lakini mzee mzima alikomaa na kufight hadi kufika alipo kwa sasa. Alipokwenda Coke studio diamond aliirudia ngoma ya "temptation" ya P-square na ni dhahiri kuwa msanii huyu anazidi kukua kila siku na kuzidi kujipanga katika level za kimataifa. 

Nani alikuja kufikiri Diamond angefanya vizuri katika nyimbo inayotumia lugha ya kigeni kama alivyofanya temtation,nadhani ili ni swali ambalo wengi walikuwa wakijiuliza kabla ya kupanda jukwaani,sio siri uwezo wake wakua flexible na kukua na kubadilika kimazingira kunamfanya Diamond kuwa kama Michael Jackson katika ukanda huu wa afrika Mashariki kama alivyosema msanii aliyefanya naye collabo hii yaani HHP.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA