Jengo likiwaka moto. JENGO la ghorofa tatu lililopo Manzese-Bakhresa jijini Dar es Salaam ambalo linatumiwa kwa shughuli za utengenezaji wa soli za viatu na lina maduka, jana lilishika moto baada ya kutokea hitilafu ya umeme ambapo vitu kadhaa vilivyokuwemo ndani yake viliteketea. Walioshuhudia moto huo ulioanza kuwaka majira ya saa saba za mchana walivilaumu vikosi vya uokoaji na zimamoto ambavyo vilichukua zaidi ya saa moja tangu moto huo uanze kuteketeza vitu katika jengo hilo. Wafanyakazi wa Tanesco wakiondoka eneo la tukio baada ya kuhakikisha umeme hauleti tena madhara eneo hilo. Mashuhuda wakishangalia tukio hilo. Gari la polisi likiwasili eneo la tukio kulinda usalama. Gari la zimamoto la kampuni ya Ultimate Security likielekea eneo la tukio. picha hizi ni kutoka tovuti y a http:// www.globalpublishers.com
Posts
REDDS FASHION SHOW
- Get link
- Other Apps
Meneja wa kinywaji cha Redds kinachozalishwa na kampuni ya (TBL) Kabula Nshimo akikaribisha wageni mbalimbali walioalikwa katika onesho hilo lililoandaliwa na kampuni hiyo kama wadhamini wenza wa Vodacom Miss Tanzania linalofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi usiku huu, Shindano la Vodacom Miss Tanzania limepangwa kufanyika Septemba 11 mwaka huu jijini Dar es salaam. Mrembo Geneviva Emmanuel akipita na kivazi cha Redds wakati wa onesho la Redds fashion Show lililofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi usiku wa jana likishirikisha warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania ambalo linatarajiwa kufanyika Septemba 11 jijini Dar es salaam. Warembo kutoka kanda ya Temeke wakipita na kivazi cha Redds. Warembo kutoka kanda ya kati ya wakipita na kivazo cha Redds. Warembo kutoka kanda ya Ilala wakipita jukwaani na kivazi cha Redds. Mashabiki mbalimbali wapo wakishuhudia onesho la Redds Fashion Show kwenye ufukwe wa Mbalamwezi. Mrembo anayemaliza muda wake Miriam Gerald wa pili
TIGO KUJENGA MINARA 8 MUSOMA VIJIJINI NA SERENGETI
- Get link
- Other Apps
Kampuni ya simu ya Tigo inajiandaa kuanza ujenzi wa minara 8 itakayojengwa maeneo mbalimbali ya Musoma vijijini maeneo ya Suguti,Makojo,na Saragana kwa upande wa Serengeti ni maeneo ya Ngoreme,Isenye na Nyichoka hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo , Dallon Kango dhumuni kubwa la kujenga minara hiyo ni kusogeza huduma zao katika maeneo hayo ,aliendelea kusema kuwa "tumeamua kujenga minara hiyo kwa sababu kwa muda mrefu sasa watu wa maeneo haya wamekuwa wakiangaika kupata huduma zetu ambazo ni nafuu sana hapa nchini ukilinganisha na mitandao mingine ya simu.
THT,AY,WAHU KUPAMBA MISS TANZANIA
- Get link
- Other Apps
Wasanii wa kundi la Tanzania Houde Of Talent (THT) wanaotamba na jimbo mbalimbali hapa nchini na Wahu kutoka Kenya wanatarajiwa kupamba shindano la Miss Tanzania linalotarajiwa kufanyika tarehe Septemba 11 kwenye ukumbi wa Mlimani City. Mratibu wa shindano Hashim Ludenga alisema kuwa mbali na wasanii hao,pia kutakuwa na burudani kutoka kwa AY,Mheshimiwa Temba,Chege na Mataluma. Shindano hilo linawashirikisha warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
UPENDO NKONE AJIANDAA KUFUNGA NDOA
- Get link
- Other Apps
Mwimbaji mashuhuri wa nyimbo za INJILI Bi Upendo Nkone ambaye amekuwa mjane kwa muda wa miaka tisa anatarajia kufunga ndoa na Mchungaji John Mbeyela oktoba 17 mwaka huu.Upendo Nkone anatarajia kuagwa oktoba 11 nyumbani kwao Kigoma,Tanzania na ndoa yake na mchungaji huyo ambaye ni mjane mwenye watoto watatu itafungwa katika kanisa la Naioth maarufu lililopo Mabibo Makuburi jijini Dar es salaam.Mwimbaji huyo aliyeanza kuimba miaka mitano iliyopita amefanikiwa kutoa albamu tatu ambazo ni Mungu Baba,Hapa Nilipo na Zipo faida .
PRECISION AIR YAONGEZA NDEGE MPYA
- Get link
- Other Apps
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.Mohammed Babu akikata utepe kama ishara ya kuzindua ndege mpya ya Precision ART 42- 500 yenye uwezo wa kubeba abiria 48 ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es salaam na Bukoba na kurudi Dar es salaam, ndege hiyo iliruka kutoka Dar es salaam kwenda Zanziar na kurudi kwa majaribio na inatarajia kuanza safari zake mwezi ujao, wanaoshuhudia katika picha kutoka kulia ni Jamal Hussein Afisa Mtendaji Mkuu Citi Bank, Allan Sharra Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air na kushoto ni Rubani wa Ndege hiyo Chohan Mbarouk Mwana blog John Bukuku wa www.fullshangwe.blogspot.com akijiandaa kushuka mara baada ya ndege hiyo kurejea Dar es salaam ikitokea Zanzibar jana. Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye alikuwa mgeni rasmi Mh. Mohamed Babu katikati akisubiri ndege itue ili kufanya uzinduzi rasmi kwa kukata utepe kulia ni Allan Sharra Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air kushoto ni Jamal Hussein
Ravalomanana ahukumiwa kifungo
- Get link
- Other Apps
Rais wa Madagascar anayeishi uhamishoni, amepewa hukumu ya kifungo cha maisha jela, na kazi ngumu kwa kutoa amri ya mauaji ya wafuasi wa upinzani. Marc Ravalomanana alihukumiwa bila ya yeye kuwepo mahakamani, kufuatia mauaji yaliyotokea mwezi Februari 2009, ya watu wasiopungua 30 na walinzi wake. Bw. ravalomanana amekuwa akiishi nchini Arika Kusini tangu mezi machi mwaka 2009. Watu waliouawa walikuwa wafuasi wa Andrey Rajoelina, ambaye hivi sasa ni rais. Bw. ravalomanana alishitakiwa kwa makosa ya mauaji na kuhusika katika mauaji, pamoja na washitakiwa wengine 18, wengine pia wakiwa wanaishi uhamishoni. Wakili mtetezi wa rais wa zamani, waliondoka mahakamani muda mfupi baada ya kesi kuanza kusikilizwa, wakisema mahakama hiyo inatumiwa na utawala wa Bw. Rajoelina "Lengo ni kumhukumu ili asiweze kurejea Madagascar na kushiriki katika uchaguzi siku zijazo," wak
Poulsen awatema Tegete, Yondani, wengine watano
- Get link
- Other Apps
KOCHA wa Taifa Stars, Jan Poulsen amewaacha wachezaji saba mahiri kwenye safari ya Algeria kwa sababu ambazo ameziita kuwa za kiufundi na ushindani mkubwa kwenye kikosi chake. Kikosi hicho cha wachezaji 20 kitakachoondoka Jumanne kwenda Algeria kwa mchezo huo wa kwanza za kusaka tiketi ya kufuzu kwa fainali za Afrika mwaka 2012. Timu hiyo itaondoka kwa ndege ya Shirikika la Ndege la Qatar Airways kuelekea Algiers. Wachezaji walioachwa ni pamoja na Uhuru Seleman, Kelvin Yondani, Juma Jabu, Abdulhalim Humoud , Jerryson Tegete, Athuman Idd 'Chuji' na kipa Juma Kaseja. Poulsen alisema wachezaji hao wameachwa kwa sababu mbalimbali za kiufundi. Alisema Chuji na Kaseja bado ni majeruhi. “Chuji amepata nafuu , lakini hajakuwa na mazoezi kwa muda mrefu, siwezi kusafiri naye kwani hawezi kucheza, hali ambayo ni sawa kwa Kaseja ambaye nimempa muda zaidi wa kupona,” alisema Poulsen. Aliongeza kuwa Abdulhalim Humud, ambaye anaichezea Simba ameachwa kwa sababu ya timu yake kuwa na viungo wan
MAKAMUZI YANAELEKEA SEATTLE 28-AUG BAADA YA KASAS CITY
- Get link
- Other Apps
BBA ALL STARS KURUKA BONGO FLEVA WIKI HII..
- Get link
- Other Apps
Jmosi wiki hii..Dj Stive B kutoka Clouds fm atachapa ngoma kali za ukweli hasa Bongo flevaz ndani ya mjengo wa BBA All Stars na kuwarusha washiriki wote mjengoni...huu ni utaratibu mpya wa BBA All Stars mwaka huu kuwafurahisha washiriki na kuwafanya wa-enjoy weekend kila j'mosi kwa kuwaalika ma-djs mbalimbali toka nchi mbalimbali za Afrika kupiga ngoma mjengoni pale...safari hii ni zamu ya Bongo na Dj aliyebahatika kupata zali hilo ni Stive B aka Skillz...kazi kwenu fans kufuatilia nini kitajili siku hiyo
KATIZA ANGA YAO UONE SHUGHULI
- Get link
- Other Apps
Ni askari wa kikosi cha kuzuia na kutuliza fujo Tanzania, Field Force Unit, (FFU) al maaruf Fanya Fujo Uone, wakiwa katika mavazi yao rasmi tayari kwa kukabiliana na purukushani zozote ambazo zinaweza kuchomoza kutokana na kutokukubaliana katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Wabunge na Raisi.
TAHADHARI KWA WAPENDA KULA KARANGA JIANI
- Get link
- Other Apps
Mfanyabiashara ndogondogo wa karanga ambaye jina lake halikujikana akiokota karanga zilizomwagika jana nje ya Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam (? na kuzichanganya kwenye zilizomo kwenye kifuko cha biashara?). Hatua hiyo inahatarisha afya za walaji kwa kuwa upo uwezekano wa kijana huyo kuziuza tena kwa wateja wake bila wao kujua kama sio salama. Mtizamaji, tizama mwelekeo wa mikono hiyo unaookota karanga, hizo zinaelekea kutupwa au kuchanganywa'mo? Ikiwa alikuwa na nia ya kuzitupa, kwa kawaida huwa tunafyagia kwa mguu kuelekea pembeni ikiwa mikono tayari imebeba kitu, ama, kile kilichobebwa huwekwa mbali na mwelekeo wa mikono au miguu huwa upande wa ardhini (kama ni kutoka kwenye sakafu) au huwa tunaacha na kusonga mbele. Matatizo ya kiafya ya magonjwa ya mlipuko vyanzo vyake ni vya aina hii kwani sehemu kinapookotwa chakula huwa imekanyagwa na viatu vilivyopita maeneo machafu sana ikiwemo vyooni na majalalani.
NAFAZI ZA KAZI MBALIMBALI
- Get link
- Other Apps
MANAGER TECHNICAL SERVICES SECTION Qualification: Holder of BSc. Engineering in Electronics and Telecommunications Apply: The Director General, Tanzania Meteorological Agency Box 3056, Dar es Salaam Details: Mwananchi, August 16, 2010. Deadline: September 02, 2010 HEAD LEGAL OFFICER Qualification: Holder of Bachelors of Law (LLB) Apply: The Director General, Tanzania Meteorological Agency Box 3056, Dar es Salaam Details: Mwananchi, August 16, 2010. Deadline: September 02, 2010 ENGINEER Qualification: Holder of degree in Engineering or Advanced diploma in Engineering (Telecommunications/Electronics) Apply: The Director General, Tanzania Meteorological Agency Box 3056, Dar es Salaam Details: Mwananchi, August 16, 2010. Deadline: September 02, 2010 REGISTRY CLERK Qualification: Holder of Advanced certificate of Secondary Education with passess in English Apply: The Director General, Tanzania Meteorological Agency Box 3056, Dar es Salaam Details: Mwananchi, August 16, 2010. Deadline: Septe
UCHAGUZI MKUU 2010: Mawaziri wanyakua ushindi mezani
- Get link
- Other Apps
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimezidi kujitwalia majimbo ya ubunge kabla ya upigajikura hapo Oktoba 31 mwaka huu, baada ya idadi ya wagombea wake wakiwemo mawaziri kupita kwa ushindi wa 'mezani' wa mapingamizi dhidi ya washindani wao na kuwezesha chama hicho, kuweka kibindoni majimbo 16 hadi sasa hivi. Hadi jana, CCM iliweza kujitwalia majimbo zaidi likiwemo Mlele kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, baada ya mgombea wa CUF Abasi Rashid, kujitoa kwenye mbio hizo huku katikia Jimbo la Mtama, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akipita kwa mlango huo wa pingamizi dhidi ya Isaya Ndaka wa TLP, baada ya kukosa idadi ya wadhamini wanaohitajika. Kasi hiyo ya CCM ilizidi kuongezeka jana baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani Lawrence Masha kupita kwa mlango huo wa pingamizi dhidi ya mshindani wake kutoka Chadema Wenje Ezekie huku Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja, naye akipeta. Hadi sasa wana CCM waliotangazwa kuteuliwa wabunge na majimbo yao kwenye mabano ni
Watanzania wanaoishi nje hawatapiga kura 2010
- Get link
- Other Apps
Serikali imesema kuwa bado haijakamilisha mkakati utakaowezesha Watanzania wanaoishi nje ya nchi kupiga kura hivyo watakosa haki hiyo katika uchaguzi mkuu utakoafanyika Oktoba 31, mwaka huu. Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe alisema kuwa, kwa sasa bado wanalishughulikia suala hilo lakini hawawezi kupiga kura kwa sababu mchakato huo bado. “Hawawezi kupiga kura watanzania wanaoishi nje ya nchi, kwa sababu suala lao bado linafanyiwa kazi, hivyo basi hawawezi kupata nafasi ya kushiriki kwenye uchaguzi huu,”alisema Membe jana alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa, Serikali bado inaendelea kuweka mazingira yatakayowezesha watu hao kupiga kura waweze kushiriki katika uchaguzi wa mwaka 2015. Alisema pindi mchakato huo utakapokamilika, Serikali itaweka hadharani ili wadau wote wafahamu namna utakavyotekelezwa kwa kuweka mazingira huru yenye lengo la kupanua demokrasia.
HAZINA YA UTALII KISIWANI UKEREWE
- Get link
- Other Apps
KATIKA POZI MASUPER STAR WA KESHO WA PANDE HIZO ZA UKEREWE MLANGO WA KUINGIA PANGO LA BENKI. KORIDO INAYOTENGANISHA PANGO LA HIFADHI (SEHEMU YA BENKI YA WATEMI) NA UKUMBI WA MAPUMZIKO. ILI KUKUZA MAENDELEO YA SEKTA YA UTALII, KAMA MCHANGO WA SEKTA HII KWA TAIFA, JUHUDI ZAIDI ZA KUBORESHA MIUNDOMBINU KATIKA VIVUTIO VYA UTALII SHURTI VIPEWE KIPAUMBELE. MUHIMU NI KWA SERIKALI NA WAENDESHA SHUGHULI ZA UTALII NCHINI, KUANDAA UTALII KWA WANANCHI ILI WAWEZE KUONA VIVUTIO NA UTAJIRI WA NCHI YAO. OF COZ' SEHEMU YA SOMO LA HISTORIA UTALII NI NJIA NYINGINE YA KUPATA ELIMU. LIKIWA NA MVUTO WA KIPEKEE HILI NI KANISA LA KWANZA LA ROMAN CATHOLIC LILILOJENGWA ENZI ZA UKOLONI KTK KISIWA CHA UKARA WILAYANI UKEREWE. H ANDEBEZYO HILL SEHEMU ILIYO JUU YA KILELE CHA KILIMA CHA PANGO LA BENKI YA WATEMI . ENEO AMBALO LILITUMIKA KWA AJILI YA ULINZI NA USALAMA WA KISIWA, KUONA MAADUI WANAOKUJA KUVAMIA NA KADHALIKA. UKISIMAMA ENEO HILI UNAONA SEHEMU KUBWA YA KISIWA CHA UKEREWE.