GARI LA BUNDA EXPRESS KUTOKA MUSOMA KUELEKEA MWANZA YAPATA AJALI

kutoka katika blog ya gsengo anasema hivi


"Eneo la katikati ya Lugeye na Nyanguge basi la abiria la 'Bunda express" lenye namba za usajili T782BKZ likitokea Musoma kuelekea jijini Mwanza muda wa saa mbili asubuhi hii limepata ajali mbaya kwenye eneo hilo, mazingira yanaonesha kuwa idadi kubwa ya watu wamekutwa na umauti na wengine kuwa majeruhi kwani gari tairi ziko juu limetumbukia majarubani, limepondeka vibaya upande mmoja, na tayari katika muda huu napita eneo la tukio miili ya watu wawili imeonekana ikizagaa nje ya basi kandokando ya barabara na mvua kubwa inaendelea kunyesha.
Chanzo cha ajali  ni mwendo kasi, watoto wakiwa na mama zao wanalia tu wakihitaji msaada, maji yamejaa hadi barabarani".

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA