Historia ya "danadana" na mabilioni yaliyopotea tangu kuanzishwa NIDA


Info Post
2/12/2016 06:39:00 AM
Mradi wa Vitambulisho vya Taifa umekuwa na historia ndefu. Ulibuniwa mwaka 1972 ikiwa ni zaidi ya miaka 38 iliyopita kwa kupitisha bungeni Sheria ya Vitambulisho na Uraia ya mwaka 1972.

Tangu wakati huo, mawaziri waliopita Wizara ya Mambo ya Ndani waliukuta na kuuacha kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo mgongano wa masilahi ya umma na ya binafsi.

Oktoba 1999 mradi huo ulitangazwa na kampuni 27 za nje na ndani ziliomba kazi hiyo. Kutokana na mizengwe, urasimu na hila za ufisadi makampuni 22 yalijitoa kwenye kinyang’anyiro hicho na zabuni ikafutwa katika mazingira ya kutatanisha.

Serikali iliipa kazi hiyo kampuni ya Gotham International Ltd inayomilikiwa na Jack Gotham aliyekuwa akishirikiana na Ofisa wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), John Kyaruzi, ambaye alisaidia kuiunganisha kampuni hiyo na Business Connections ya Afrika Kusini na kwa pamoja wakashughulikia ‘mchanganuo’ wa mradi huo.

Mabilioni yanavyopotea

Ripoti mbalimbali zinaonyesha Serikali imepoteza karibu Sh bilioni 500 kwa miaka tisa kutokana na matumizi mabaya ya fedha za umma ikiwamo rushwa na ubadhirifu wa mali mbalimbali.

Hiyo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia katika moja ya ripoti zake alizowahi kuzitoa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk. Helen Kijo-Bisimba.

“Katika kipindi kisichozidi miaka tisa kumeripotiwa kashfa kubwa nne ambazo kwa ujumla wake zimelisababishia Taifa hasara ya karibu Sh bilioni 500 ambako kwa wastani inapoteza takriban asilimia 20 ya bajeti yake ya mwaka,” alisema Sungusia.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA