Waziri Ummy aagiza watumishi 4 MSD wasimamishwe kazi mara moja

2/15/2016 07:21:00 PM
Waziri Mwalimu na Katibu wa Wizara ya Afya, Dk Ulisubisya

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu ameagiza Wakurugenzi wa Bohari ya Dawa ya Taifa (MSD) waandikiwe barua mara moja ya kusimamishwa kazi kutokana na tuhuma za kukiuka taratibu za manunuzi na ubadhirifu wa fedha takribani shillingi bilioni 1.5/=.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto baada ya kupokea vifaa toka Bohari Kuu ya Dawa ya Taifa (MSD), ambapo amesema amechukua hatua hiyo kwa kuzingatia taarifa ya uchunguzi ofisini kwake.

“Nimepata taarifa toka ofisini kwangu na nimeamua kuchukua fursa hii kuwaambia na hili pia kwamba nimewasimamisha Wakurugenzi wanne toka Bohari ya Kuu Dawa ya Taifa. Nisingeweza kusubiri nitumbuliwe mimi jipu na Mhe. Rais. Kwa hiyo nimeamua kuwachukulia hatua kwa kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi.”

“Hizi ni zama za kufanya kazi na kuwajibika sasa inabidi tuwajibike kwa kufanya kazi na hatutowavumilia watendaji watakaoenda kinyume na utaratibu katika ofisi yoyote ile katika sekta ya afya na tutawachukulia hatua kwani tunataka uwajibikaji ili kuiendeleza sekta ya afya ambayo ni muhimu sana kwa kila mwanadamu” Alisema Ummy.

Amewataja aliowasimamisha kazi kuwa ni Joseph Tesha Mkurugenzi wa Fedha na Mipango, Misanga Muja Mkurugenzi wa Ugavi, Heri Mchunga Mkurugenzi wa Manunuzi na Cosmas Mwaifani Mkurugenzi Kanda na Huduma kwa Wateja ambapo amewataka Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bohari ya Dawa ya Taifa.

Katika kuboresha sekta ya afya nchini Wizara wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee imejipanga kufanya kazi kwa taratibu na misingi iliyopo ili kuhakikisha inapeleka mbele gurudumu la maendeleo ya hasa katika sekta ya afya kwa ujumla.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA