Wanne wasimamishwa; Mkurugenzi apewa saa 48 na NW TAMISEMI kueleza ziliko milioni 180/=


SELEMAN Jafo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, amebaini upotevu wa Sh 180 milioni katika halmashauri ya wikaya ya Kondoa mkoani Dodoma.

Kutokana na kubainika kwa upotevu wa fedha hizo Jafo ametoa saa 48 kwa Hussein Issa ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, kuhakikisha anapeleka maelezo ya kina katika Ofisi ya TAMISEMI juu ya kuibiwa kwa fedha hizo ambazo ni za walipakodi watanzania.

Agizo hilo la Jafo lilitokana ziara ya kikazi iliyofanywa na naibu waziri huyo sambamba na kufanyika kwa kikao cha ndani katika Halmashauri hiyo.

Amesema, Serikali ya Awamu ya Tano haitavumilia kiongozi yoyote ambaye atafanya ubadhilifu kwa fedha ya Umma au jambo lolote ambalo linaonekana kuwepo na alufu ya ufisadi.

Amesema nchi imekuwa ikiendeshwa kimazoea na watu kujilimbikizia mali bila kuwa na hofu ya kuhojiwa jambo ambalo liliwafanya watumishi wa Umma kuwa na kiburi na kufanya kile wanachofikiria.

“Nchi imekuwa ikiendeshwa kimazoea sana watu wanakula hela bila utaratibu na wanafunika funika tu mambo huku wakiwafanya watu kama vipofu, hili haitavumiliwa hata kidogo lazima hatua stahiki zichukuliwe,” amesema.

Jafo amesema, anataka maelezo ya kina juu ya wizi wa fedha hizo na ndani ya saa hizo 48 anataka awe amepata taarifa ofisini kwake.

Sambamba na hilo, aliagiza watu nane wanaotuhumiwa kuhusika na wizi wa fedha hizo wasimamishwe kazi na kukaa pembeni kupisha uchunguzi.

Aidha, amewaagiza maofisa utumishi na wakuu wa idara kuwajibika na kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.

Naibu wiziri huyo ameeleza kuwa kumekuwepo na malalamiko mengi juu ya watendaji we ngazi ya chini ambao wamekuwa wakionewa na kutopatiwa haki zao kama inavyostahili.

Amesema, watumishi hao wanalalamika kutolipwa malimbikizo yao mbalimbali kama fedha za likizo na kutopandishwa vyeo kwa wakati.
  • via MwanaHALISI Online

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA