Vodacom yatoa ofa ya internet Bure

Kampuni ya Simu za Mkononi ya VodaCom Tanzania, imezindua huduma mpya ya intaneti ambayo itawawezesha wateja wake kulonga (chat)kwa intaneti bure.

Mkurugenzi wa Uhusiano wa VodaCom Tanzania, Mwamvita Makamba amesema kuwa wateja wa VodaCom sasa wanaweza kuwasiliana zaidi kwa kulonga bure kwenye tovuti za FaceBook, TheGrid na VodaMail. Huduma hiyo itapatikana kwa simu za mkononi na pia kwa Laptop zilizounganishwa na USB Moderm.

“Tunapenda wateja wetu watumie mtandao wetu kwa kuwasiliana bure na hivyo kukata kiu yao ya mawasiliano”.

Alifafanua kwamba hayo yote yatawezekana kwa kutumia mtandao wa 3G ambao una kasi na nguvu kubwa.


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA