tigo yaichangia ccrbt kuendeleza huduma bure.

Jumla ya watoto 160 watapatiwa huduma ya upasuaji wa macho katika kliniki maalum ya huduma hiyo zitakazoendeshwa na Shirika lisilo la Kiserikali la CCBRT kwa siku 11, kuanzia Novemba 8 - 19, 2010 katika hospitali ya Sekou Toure mjini Mwanza. Shughuli hizo zitakuwa zinafanyika mara mbili kwa mwaka ambapo zoezi la pili linatarajiwa kufanyika Julai mwakani. Tigo pia itafadhili mafunzo ya wiki mbili ya kozi ya huduma za uzazi (BEmONC) kwa wakunga 10.

Mkurugenzi Msaidizi wa CCBRT bi. Haika Mawala alisema kuwa 80% ya upofu unaweza kutibiwa au kuzuiwa na ni muhimu kuwafikia watoto wengi waliozaliwa na mtoto wa jicho nchini Tanzania.

"Ninafurahi kuwa tiGO inatambua kazi ya kubadilisha maisha ambayo CCBRT inafanya katika jamii hapa jijini Dar na kwingineko," alisema Haika na kuongeza, kupitia ushirika huo muhimu sana mkoani Mwanza, watoto wapatao 160 ambao wangepata upofu watapata kuona na hivyo kuweza kuishi maisha mema zaidi.
Picture
Mkuu wa kitengo cha Udhibiti wa Mawasiliano ya Mambo ya Nje wa MIC Tanzania Ltd. Alex Kamara akimkabidhi Mkurugenzi Msaidizi wa CCBRT Haika Mawala hati ya makubaliano ya kampuni hiyo kutoa sh. milioni 76 na mchanganuo wa mradi wa ushirikiano. Tukio hili lilifanyika leo katika ofisi za CCRBT Msasani, Dar es Salaam.



Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA