MAKALA MAALUM KUTOKA KWA MDAU KUHUSU MIFUKO YA JAMII
IMEANDALIWA NA Davis Muzahula , Mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya sheria (mwaka wa nne), Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Augustino cha Tanzania Simu: +255756829416 Barua pepe: davismuzahula@yahoo.com UTANGULIZI Kwa mujibu wa Shirika la Kazi Duniani, Mfuko wa hifadhi ya jamii ni mfumo ambao jamii husika imejiwekea kwa lengo la kuwakinga watumishi wa umma au binafsi ( waajiriwa ) dhidi ya matukio yasiyotarajiwa ( Contingencies ). Matukio hayo ni kama maradhi, ulemavu, kupoteza kazi, kuacha kazi kwa sababu ya uzee ( kustaafu ) aidha kwa hiari au kwa lazima, na mengineyo ikiwamo huduma za matibabu, ghalama za msiba ikiwa mteja atafariki au kufiwa na mtu ambaye mfuko husika huchangia. Vile vile iwapo mteja atafariki kabla ya kustaafu basi mafao yake hulipwa kwa warithi wake ambavyo huweza kusaidia kusomesha watoto wa mhusika. Hifadhi kutoka kwa jamii ni haki ya kila mtu kama ilivyotajwa na katiba ya jamhuri ya Muungao wa Tanzania, 1977 (kama ilivyofa...