Pigo jingine CCM: Mbunge Eugene afariki Dunia, bunge lahairishwa


Mbunge wa jimbo la Ukonga Dar es Salaam kupitia tiketi ya (CCM) Eugen Mwaiposa amefariki dunia usiku wa kuamkia jana akiwa usingizini nyumbani kwake Dodoma.

Kwa mujibu wa Naibu Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai ambaye amelitangazia bunge jana majira ya saa 7 mchana, marehemu Mwaiposa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu kwa muda mrefu.

Ndugai amesema kuwa kwa sasa msiba upo nyumbani kwake eneo la Chadulu Dodoma ambapo pia familia yake inasubiria hapo kwa ajili ya kuaga mwili wake shughuli ambayo itafanyika leo(Jumatano).

Bunge liliahirishwa hadi kesho saa 3 Asubuhi.

Mungu ametoa Mungu ametwaa jina lake lihimidiwe. R.I.P ‪

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA