Millem Magese atunukiwa tuzo ya heshima ya Global Good ya BET Awards 2015

Miss Tanzania, 2001, Happiness Millen Magese, hatimaye ametunukiwa tuzo ya kwanza ya heshima ya Global Good ya BET Awards 2015.

Millen amepewa tuzo hiyo kutokana na jitihada zake za kampeni ya ugonjwa wa endometriosis ambao pia amekuwa nao katika maisha yake yote tangu awe msichana. Tatizo hilo limempelekea kuwa mgumba.

Pamoja na hivyo Millen amekuwa mstari wa mbele kutoa misaada mbalimbali kwa wasiojiweza.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA