Posts

Showing posts from May, 2010

FACEBOOK MAKE COMMUNICATION EASIER FOR EVERYONE INTRODUCED VIDEO CHART

Image
Video, audio, and text chat with your friends - Have them talk to you right from Video Chat on your profile. If they have Video Chat too, just have them click 'Talk to me' under your profile. Invite friends who also have Video Chat right into the conversation from the Video Chat application. Schedule times for you and your friends to meet up at your chat room. You can share YouTube videos and watch them with your friends by sending a YouTube URL to your friends in the text chat window. The YouTube video starts playing in a new window in the application. Your friends can record new audio and video messages for you when they come looking for you and if you are not present in your room. You friends can also view messages left for you in your room. You are alerted on your instant messenger of choice when someone visits your room. Your visitors can send you a personalized text message that you will receive on your instant messenger when someone visits your widget. You can click on t...

Brazili kucheza na Taifa Stars ya Tanzania Juni 7 05/27/2010

Image
Brazili kucheza na Taifa Stars ya Tanzania Juni 7 05/27/2010 Timu ya soka ya Brazili ambayo imeshawasili nchini Afrika Kusini tayari kwa mashindano ya kuwania Kombe la Dunia la Soka, inatarajiwa kuingia nchini Tanzania Juni 5 kwa ajili ya mechi ya kirafiki na Timu ya soka ya Tanzania ya Wanaume, Taifa Stars hapo Juni 7, 2010. Balozi wa Brazili nchini Tanzania, Francisco Carlos Soares Luz amesema timu hiyo itawasili na nyota wake wote watakaoshiriki katika fainali hizo.

NITASOMA SCHOLARSHIP WINNERS MAY 2010

Image
RENILDA AMBROSE CHIMA FULL DURATION SCHOLARSHIP CHIMALA HIGH SCHOOL MBEYA Other winners include; 1.SUSAN MILANZI NITASOMA LAPTOP 2 2.JOYCE MARUWA NITASOMA STATIONERY INSTITUTE OF SOCIAL WORK (HRM) 3RD YEAR 3. SAADA S SADALA NITASOMA MOBILE T.I.A BBA 1ST YEAR

MACHOZI BAND WAAMISHA ,MAKAZI TO MZALENDO PUB KILA FRIDAY

Image
GOOD NEWS KWA WAPENZI WA MACHOZI BAND IJUMAA HII.......KIWANJA KITAKUWA MZALENDO PUB EVERY FRIDAY Machozi Band sasa wamehamia mzalendo pub sehemu yenye upepo wa asili wa kutosha bila kuhitaji mafeni.......... Ni Mzalendo Pub, kuanzia Ijumaa ya tar 28 May 2010 na Ijumaa nyingine zote zitakazofuata Karibuni mu enjoy, na samahanini tena kwa kuwakosesha burudani Ijumaa iliopita Alhamisi ni Savannah Lounge kama kawaida na Jumapili ni Thai Village

Tiketi za WOZA 2010 kwa Tanzania zawasili

Image
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Florian Kaijage kizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusiana na utaratibu wa kupata tiketi zilizoletwa na FIFA ili kushuhudia baadhi ya michezo ya Kombe la Dunia. Kwa sababu za kiusalama na uthibitisho, watu wote walionunua tiketi hizo wanahitajika kuwa na risiti zao pamoja na picha ndogo 'Passport Size' ili waweze kupatiwa tiketi zao

Wafanyakazi WOTE wa ATCL waachishwa kazi

Image
Kamati ya kudumu ya Bunge na Fedha na Uchumi iliyokutana jijini Dar Es Salaam tarehe 25 Mei 2010 imeridhia mapendekezo na ushauri wa Ofisi ya Msajili wa Hazina la kuwaachisha kazi Wafanyakazi wote wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ili kuipunguzia mzigo Serikali. Ushauri huo umetolewa na mshauri wa Msajili wa Hazina bwana Godfrey Msella na kusema, "kama ATCL haibebeki, ni bora Serikali ibwage manyanga" na hivyo kufuatiwa na tamko rasmi la Mwenyekiti wa tume hiyo ya Bunge, mhe. Abdallah Kigoda. Hatua kama hiyo iliwahi kuchukuliwa katika shirika la Bima la Taifa (NIC) na imependekezwa kuwa hatua hii isiichie ATCL pekee bali ifike pia katika Shirika la Reli nchini (TRL). habari hii ni kwa hisani ya tovuti ya www.wavuti.com

TWANGA KUSUGUA KISIGINO MBEYA NA IRINGA.

Image
Bendi ya muziki wa Dansi ya African Stars maarufu kama Twanga Pepeta iliyo na maskani yake jijini Dar, inatarajiwa kufanya ziara maalum katika mikoa ya Iringa na Mbeya ili kuwashukuru mashabiki wa mikoa hiyo miwili kutokana na kuipigia kura kwa wingi na kufanikiwa kuchukua tuzo tatu za KILI kwa mwaka huu. Ziara hiyo inatarajiwa kuanzia katika Mkoa wa Iringa siku ya Alhamisi ya tarehe 3 mwezi wa sita katika Club ya V.I.P, na siku inayofuata ya tarehe 4 mwezi wa sita Twanga pepeta itamalizia ziara yake katika ukumbi wa Mkapa uliopo katikati ya Jiji la Mbeya. Maonyesho yote mawili yanatarajia kuanza saa mbili za usiku na kwa Mkoa wa Iringa, Twanga pepeta inataraji kusindikizwa na Bendi ya Sweat Noise iliyo na maskani yake Iringa. Twanga pepeta itaitumia ziara hiyo ya mikoa ya Iringa na Mbeya kuwadhihirishia mashabiki wa Mikoa hiyo kwamba Twanga Pepeta iko juu na wanataraji kusafiri na kikosi kizima kilicho na nyota wote wakiongozwa na Kiongozi Mkuu mamaa Luiza Mbutu na wengineo kibao. Aid...

RIP JUSTINE KARIKAWE

Image
Habari nilizozipata kutoka katika blog ya changamotoyetu.blogspot ni kuwa yule gwiji wa mziki wa regee nchi Justine karikawe amefariki.

Aliyenusurika Katika Ajali ya MV Bukoba Atunga Kitabu Kuhusu Kitukio Hilo.

Image
Mmoja wa wahanga waliokoka katika ajali ya Mv Bukoba iliyotokea Mei 21 siku ya Jumanne mwaka 1996 Nyaisa Simango ambaye kwa sasa ni Afisa Ugavi wa Benki Kuu ya Tanzania akionyesha kitabu alichotunga baada ya kunusurika katika ajali hiyo iliyouwa watu 800. Nyaisa kipindi hicho alikuwa mwajiriwa wa jeshi la Magereza kituo cha Ukonga jijini Dar es Salaam, wakati tukio linatokea alikuwa amempeleka mfungwa mkoani Kagera, kitabu hicho alichozindua kina kurasa 167, kikiwa na kichwa cha habari kisemacho SITASAHAU MV BUKOBA. Kulia ni Afisa habari mwandamizi wa Habari Maelezo Mwirabi Sise pia ni Mjomba wa Nyaisa kitabu kinapatikana katika bookshop mbali mbali hapa nchini kwa shilingi 12,000.

OFID SCHOLARSHIP AWARD 2010/11

OFID SCHOLARSHIP AWARD 2010/11 CALL FOR APPLICATIONS OFID (The OPEC Fund for International Development) is pleased to announce that qualified applicants who have obtained or are on the verge of completing their undergraduate degree and who wish to study for a Master's degree are welcome to apply for the OFID Scholarship 2010/2011. The OFID scholarship will be awarded to support one student or candidate for Master’s degree studies. The applicant may be from any developing country, and he/she must first obtain admission to pursue a Master's degree studies in a relevant field of development, in any recognized university/college in the world. Through its scholarship scheme, OFID aims to help highly motivated, highly-driven individuals overcome one of the biggest challenges to their careers – the cost of graduate studies. The winner of the OFID Scholarship Award will receive a scholarship of up to US$100,000. The funds will be spread over a maximum of two years, toward the completio...

TID asema Hasheem Thabeet amempiga!

Hizi habari za "watu maarufu nchini Tanzania" kutafautiana na hatimaye kuzuliana magomvi yanayoishia kupigana si nzuri hata kidogo. Tabia hii ni mbaya kabisa katika jamii kwani inaendeleza habari za visasi ambavyo siku zote si tija katika kujenga maisha. Yeyote anayedhani ugomvi ni mtajiwa mafanikio, sidhani kama anatofauti na mtu anayepokea ujira wa haramu na damu. Watu wanaofahamika zaidi katika jamii wanapoamua kufanya vibweka hadharani badala ya kuwa mfano bora, huwa wameiajisi heshima waliyotunukiwa na jamii husika, na hii ni dharau. Haifai hivi. Habari ifuatayo imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya TID (Top In Dar - mojawapo ya wanamuziki wa kizazi kipya - Bongo Fleva/Fleva) anayedai kupigwa na Hasheem Thabeet (Hashim Thabit - Mtanzania wa kwanza kufanikiwa kucheza ligi ya mpira wa kikapu al maaruf NBA huko nchini Marekani). TID Anasema Ilikua majira ya saa kumi unusu nikiwa natoka club billcanas pamoja na rafiki yangu ANNA tukiongozana kuelekea mlango mkubwa wa kioo nikiw...

ongezeko la maambukizi mapya ya ukimwi kisiwa cha Rukuba yazidi kushika kasi

Kisiwa kilichopo katika ziwa victoria mkoani Mara katika wilaya ya Musoma vijijini cha zidi kupamba moto katika maambukizi mapya yanayozidi kusambaa kwa wakazi wake ambao asilimia 90 ni wavuvi .Katika taarifa niliyoipata leo katika kituo kimoja cha radio ni kuwa wanakijiji wengi wa eneo hilo wanazidi kuteketea kwa gonjwa hili hatari kwa sababu ya kukosa elimu ya kutosha juu ya gonjwa hili sababu hii ilitolewa na tabibu mkuu wa zahanati iliyopo katika kisiwa hicho.Hatua kubwa inatakiwa kuchukuliwa zaidi na Mashirika mbalimbali yanayojihusisha na kutoa elimu ya Ukimwi.

AJALI NYINGINE TENA PWANI

Image
Watu watano wamefariki dunia baada ya kutokea ajali iliyosababishwa na malori mawili ya mafuta kugongana uso kwa uso kisha kulipuka leo Mei 6, 2010 saa mbili asubuhi eneo la Vigwaza mkoani Pwani. Taarifa zinasema kuwa gari lililokuwa limebeba kontena liliharibika eneo hilo, kwa hiyo wakawa wanatengeneza. Utingo na dereva wake waliingia uvunguni kupiga jeki, ndipo gari lingine la kampuni hiyo likafika na dereva akashuka wakawa wanasaidiana. Wakiwa wanatengeza gari hilo, likaja lori lenye mafuta likitokea Dar es Salaam na lori lingine lisilo na mafuta likitokea Morogoro. Lori la Dar es Salaam likiwa katika mwendo kasi lilikuwa almanusura ligongane uso kwa uso na lile llilotokea Morogoro ndipo katika kukwepana, lori mojawapo likagonga kontena kwa nyuma na kusababisha jeki kufyatuka na kuwakandamiza watu watatu ambapo utingo aliaga dunia papo hapo. Madereva walifia njiani wakati wakikimbizwa hospitali ya Tumbi Kibaha kwa matibabu. Pia, cabin ya lori lililokuwa likitoka Dar es Salaam iliwak...

Nigerian President Umaru Yar'Adua has died

Image
RIP Umaru Yar'Adua Nigeria's ailing President Umaru Yar'Adua has died on Wednesday at the age of 58, the country's Information Minister, Dora Akunyili said. Yar'Adua had not been seen in public since November, when he went to Saudi Arabia for treatment of pericarditis (inflammation of the heart muscles). He was diagnosed with the condition, acutely, at the end of last year after he complained of chest pain, he also developed kidney problems.

Dar Mvua Ni Karaha!

Image
Leo alfajiri wakazi wa Dar Es Salaam wameamshwa na mvua kubwa iliyonyesha kwa zaidi ya saa moja na nusu. Bado inanyesha lakini imepungua kasi baadhi ya picha. Hizo ni kwa hisani ya mjengwa!

JK akiwachimba mkwala Tucta

Sitisho la Mgomo uliokuwa umeitishwa na TUCTA

Image
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Ayubu Omary na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Nicholas Mgaya, wamezungumza na vyombo vya habari tarehe 4 Mei 2010 katika ukumbi wa shirika la kazi la Umoja wa Mataifa, ILO, na kueleza nia yao ya kusitisha mgomo uliokuwa uanze tarehe 5 Mei 2010 nchini kote. Wamesema wanamuamini Mh Rais Jakaya Kikwete ila wamelaumu kutokutendewa haki katika hotuba yake aliyoisoma kwa Taifa alipozungumza na Wazee wa Dar Es Salaam. Hivyo, bwana Mgaya amewataka Wafanyakazi wote kuendelea na kazi kama kawaida na kuwa mgomo huo umesitishwa na hautakuwepo tena mpaka itakapotangazwa vinginevyo pale watakapokutana na Serikali hapo tarehe 8 Mei 2010 kwa majadiliano zaidi. Wamesema wana amini kwamba masuala yao ya mishahara na kodi zinaokatwa kwa Wafanyakazi vinaweza kupatiwa ufumbuzi katika kikao hicho. habari hii ni kwa hisani ya www.wavuti.com

Mlimani City inavyoonekana kwa nje tayari kwa WEF

Image
Hili ni eneo la nje, sehemu ambamo upo ukumbi wa Mlimani City ambao kesho utatumika kwa ajili ya Mkutano wa Dunia wa Kiuchumi kuhusu bara la Afrika (World Economic Forum on Africa - WEF) Mkutano utaanza rasmi siku ya Jumatano tarehe 5 Mei 2010 hadi Ijumaa, Mei 7, 2010. Mapambo ya kupendezesha barabara watakakopita wageni ni pamoja na usimamishaji wa miti ya Minazi katika barabara ya Sam Nujoma kuanzia eneo la Mwenge hadi Ubungo. Inasemekana kuwa miti hiyo imepandikizwa kwa thamani ya Shilingi 700,000/= kwa kila mmoja.

HII KALI YA MWAKA

Image
Umeona jinsi jamaa alivyo modify matumizi mapya ya masikio yake?

Basi la Islam laua wanne Morogoro

Habari nyingine za kusikitisha katika wiki hii zinatoka Morogoro zikisema kuwa basi la usafiri la kampuni ya Islam linalofanya safari zake kati ya mkoa jirani ya Dar Es Salaam na Morogoro limesababisha ajali na kuua watu wanne, akiwamo mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Gwata, Morogoro. Mwanafunzi huyo, Dotto Issa (16), alikuwa amepakiwa katika pikipiki iliyokuwa inaendeshwa na Karim Selemani ambaye pia alifariki dunia katika ajali hiyo. Kamanda wa Polisi mkoa, Thobias Andengenye amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea katika kijiji cha Lukole, wilayani Morogoro. habari hii ni kwa hisani ya tovuti ya www.wavuti.com