TID asema Hasheem Thabeet amempiga!

Hizi habari za "watu maarufu nchini Tanzania" kutafautiana na hatimaye kuzuliana magomvi yanayoishia kupigana si nzuri hata kidogo. Tabia hii ni mbaya kabisa katika jamii kwani inaendeleza habari za visasi ambavyo siku zote si tija katika kujenga maisha. Yeyote anayedhani ugomvi ni mtajiwa mafanikio, sidhani kama anatofauti na mtu anayepokea ujira wa haramu na damu.

Watu wanaofahamika zaidi katika jamii wanapoamua kufanya vibweka hadharani badala ya kuwa mfano bora, huwa wameiajisi heshima waliyotunukiwa na jamii husika, na hii ni dharau. Haifai hivi.

Habari ifuatayo imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya TID (Top In Dar - mojawapo ya wanamuziki wa kizazi kipya - Bongo Fleva/Fleva) anayedai kupigwa na Hasheem Thabeet (Hashim Thabit - Mtanzania wa kwanza kufanikiwa kucheza ligi ya mpira wa kikapu al maaruf NBA huko nchini Marekani). TID Anasema

Ilikua majira ya saa kumi unusu nikiwa natoka club billcanas pamoja na rafiki yangu ANNA tukiongozana kuelekea mlango mkubwa wa kioo nikiwa naongea na simu na Hisbert kwa sauti ya juu maana kelele za muziki zilikua zinasumbua nikiwa nimesimama nje ya mlango wa kioo ghafla akatokea bwana HASHIM ambaye alikua counter akiongea na wakata ticket akaja nje na kunipiga bonge la mtama nikaaunga chini ya sakafu na kuzirai kwa dakika kadhaa,mabaunsa wakanibeba na kuniweka pembeni maana nilikua mlangoni,nilipozinduka nilisikia maumivu makali kwenye mabega,mkono wangu wa kulia na mguu ambao unafanya kutembea kwangu kwa taabu,nikaangalia mkononi simu yangu sikuiona tena,nikawauliza mabaunsa wake jamaa amekwenda wapi!wakadai ameondoka tayari...nikajikokota kuelekea kwenye gari yangu na kuelekea polisi kutoa taarifa niweze kupata matibabu,nilipofika nikaaandika statement nikapewa namba ya case CD/RB/6848/10 pia nikapatiwa PF3 nikaenda hospitali nikapata matibabu,sasa hivi niko kitandani siwezi kutembea vizuri,pia nitashindwa kuperfom kwenye harusi ambayo tayari nishalipwa pesa tayari.SWALI langu ni kwanini ameamua kunidhalilisha vile mbele ya CLUB na FANZ ambao nilikua nawatumbuiza?kwanini ameamua kuniharibia kazi yangu?kwanini ameamua kunipiga bila ya kumkosea?JE NI SAWA HIVI JAMANI....naona MACHOZI YANANITOKA SINA CHA KUMUELEZA MAMA YANGU.

...kwa habari ambazo zipo chini ya kapeti kitaa ni kua inavyosemakana ANNA ambae ni rafiki yake TID aliekua nae club billcanas ndio chanzo cha ungonvi huo baada ya dem kutaka kumsalimia HASHIM THABEET na TID kukerwa na tukio hilo na akamletea dharau flani ndio akaamua kumpiga...

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA