CHRISS BROWN AWATUSI WANAO MBEZA


Kutokana na ushindi wa Tuzo ya Grammy aliyoipata wiki iliyopita jina la Chriss Brown limekuwa likipamba vyombo mbalimbali vya habari lakini watu wengi wamkuwa wakimbeza na kudai kwamba hakustahili kupata tuzo hiyo.
Hata mastaa Miranda Lambert na Jack Ousbourne waliandika katika mtandao wa twitter kuelezea mshangao wao juu ya ushindi wa kijana huyo.
Inadaiwa siyo kwamba hajui kuimba,bali ni kutokana na tukio alilofanya miaka miwili iliyopita la kumpiga mpenzi wake wa zamani,Rihana wakati wa Tuzo hizo zikiendelea kutolewa.
Lakini Chriss Brown amewatolea maneno makali wote wanaopinga ushindi wake, huku akijitetea na kusema kuwa kila mtu anastahili kupewa nafasi ya pili pale anapokosea.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA