HIVI NDIVYO MATAPELI WANAVYOSUMBUA WATAFUTA AJIRA.

Si mara ya kwanza kusikia mtu akilalamika juu ya kutapeliwa kiasi fulani cha pesa anachokitoa ili aweze kupata kazi katika ofsi fulani.

Kutokana na matatizo ya ajira hapa nchini na dunia kwa ujumla matapeli nao wanatumia mwanya huo kuakikisha  wanapata pesa kirahisi kabisa, mfano mmoja wapo ni hii messaji ambayo mimi mwenyewe nimetumiwa kwenye simu yangu.
 
"Habari, naitwa Mr. Raymond from EUROCARTA LTD Dar, tupo kikaoni tunapitia CV tuchague candidates wa kuinterview for FINANCE OFFICER POST, salary ni 1,200,000/=. CV yako ni nzuri nataka kukusaidia upate hii kazi, kwa terms zifuatazo, ukishaanza kazi utanipa laki 3, na kabla ya saa 9 mchana uwe umetuma sh. elfu 40 by tigopesa to 0713-765442 ili nimpe mtu wa interview amesema anataka hiyo hela leoleo ili atoe maswal ntakutumia kwenye e-mail for now siwezi ongea mpaka badae nikitoka kikaoni na ndio muda huo utapigiwa simu lini uje for interview, jitahidi utume mapema".

Comments

  1. matapeli pia wanatakiwa kufikishiwa habari njema za Kristo#

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA