Skip to main content

CONGO WAAMUA KUTUMIA TRAFIKI ROBOTI,SABABU HIZI HAPA

Nchi za kiafrika zikiwa zinaendelea kukumbana na tatizo la ongezeko la magari inayosababisha foleni kubwa,ambapo kwa tafiti inaoneka mji mkuu wa Angola ambao ni Luanda una foleni kubwa sana kuliko hata hii ya Dar Es Salaam.

Jiji la kinshasa ambalo pia limekuwa katika miongoni mwa majiji ambayo yako katika shida kubwa ya ongezeko la magari na kusababisha foleni kubwa inayosababisha kurudisha maendeleo ya kiuchumi pamoja na kuwa katika machafuko, wamekuja na mbinu mpya ya kutumia roboti kama trafiki.

Trafiki huyu roboti ameunganishiwa vifaa vya kisasa katika kupambana na askari wala rushwa,madereva wote wafanya makosa wawapo barabarani lakini pia kupunguza foleni kwa haraka zaidi, roboti hili limeunganishwa kwenye mfumo ambao inaweza kupiga picha na kuituma makao makuu ya polisi kwa matukio yote yanayotokea barabarani kwa muda muafaka.

Kinshasa
picha ya AFP/Getty 

Mara baada ya roboti kupiga picha, linatuma kwenye internet kwenye makao makuu ambapo mfumo wake wa mawasiliano unakuwa umesetiwa kupokea taarifa hizo zote kwa ajili ya kufanya uchunguzi zaidi.

Robot hizi zimekuja muda muafaka kwani madereva wengi wa nchi ya Congo wamekuwa wakilalamika sana juu ya matrafiki wazembe na wala rushwa
,

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA