Posts

Showing posts from July, 2015

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) YAONGEZA MUDA WA KUJIANDIKISHA JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa inaongeza muda wa siku nne tu wa kuandikisha wapiga kura kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam. Hii inamaanisha kuwa zoezi hilo ambalo lilikuwa linaisha ijumaa ya kesho julai 31, litaendelea hadi jumanne agosti 4 Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa hataweza kuongeza muda wa zaidi ya siku nne kwa kuwa rat iba zitaingiliana. Aidha, Jaji Mstaafu Lubuva amesema mpaka sasa watu zaidi ya milioni 18 wameandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa njia ya mfumo wa kielektroniki BVR kwa nchi nzima.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS, JULY 30

Image

MFANYABIASHARA NDOGODOGO ASHINDA UBUNGE VITI MAALUMU MKOA WA MARA

Image
na shomari Binda MCHUUZI wa dagaa kwenye soko la Mwigobero lililopo Manispaa ya Musoma,Agnes Methew,ameibuka mshindi wa kwanza kwenye kura za maoni za kutafuta Mbunge wa viti maalumu(CCM) mkoa wa Mara. Akitoa shukrani kwa wajumbe wa mkutano wa uchaguzi mara baada ya kutangazwa mshindi na msimamizi wa uchaguzi huo,Samwer Kiboye ambaye ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rorya,alisema wajumbe wameonyesha namna ambavyo hata mtu wa chini anaweza kushinda tofauti na inavyozungumzwa. Alisema wao watu ambao wamekuwa wakizungumza pembeni ukiwa Chma cha Mapinduzi huwezi kupata nafasi ya uongozi kama hauna fedha jambo ambalo sio kweli kwa kuwa yeye amechaguliwa bila kujali kipato chake na kuwashinda walioonekana na kipato cha juu na majina makubwa. “Niwashukuru sana wajumbe kwa kunipigia kura za kishindo na kunifanya niibuke mshindi kati ya wagombea wengine 9 wanachma wenzangu ambao nilikuwa nikishindana nao ndani ya uchaguzi huu. “2010 nilikuja kwa...

HAPPY BIRTHDAY TO ME

Image
Ni mengi napitia lakini Mungu unaendelea kunisimamia, nashukuru kwa kuwa ni mzima, naishukuru familia yangu, marafiki zangu wote ambao siku zote wamekuwa mstari wa mbele kunipa ushauri na kuniongoza pale napohitaji msaada wao, ninaamini hazina ya marafiki. happy birthday to me.

Rais Obama amaliza ziara yake Kenya

Image
Rais Obama akiwaaga Wakenya wakati akiondoka. Obama akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta tayari kuondoka. Obama akiagana na Rais Uhuru Kenyatta. Mama Sarah Obama akiwa tayari kumuaga Obama. RAIS wa Marekani, Barrack Obama jana jioni amekamilisha ziara yake ya siku tatu nchini Kenya ambapo alifungua kongamano la kibiashara, akawahutubia Wakenya katika Uwanja wa Kasarani na baadaye kuzungumza na viongozi wa mashirika ya kijamii katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Baada ya kukamilisha ziara yake hiyo, Rais Obama sasa anaelekea nchini Ethiopia kwa ziara ya siku mbili ambako anatarajiwa kuzungumza kuhusu maendeleo ya eneo hilo.

Breaking News: Bobbi Kristina mwanawe Whitney afariki

Image
Bobbi Kristina Brown ,mtoto wa marehemu Whitney Houston ambaye alikuwa gwiji wa muziki wa R&B ,amefariki dunia baada ya kupoteza fahamu kwa muda wa miezi sita tangu alipokutwa taabani kwenye bafu lake na pindi alipofikishwa hospitalini na kukutwa na matatizo kwenye ubongo. Bobbi amekufa akiwa na umri wa miaka 22,huku akivutiwa kuwa muigizaji na muimbaji mahiri na mwenye ubora wa aina yake. Msemaji wa familia Kristen Foster amesema Bobbi amefariki akiwa amezungukwa na familia yake ,''hatimaye yuko salama sasa kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu,tunawashukuru wote walioungana nasi katika maombi na kuonesha upendo kwa miezi michache iliyopita''. Bobbi ambaye alikuwa amepoteza fahamu tangu akutwe ameanguka kwenye bafu lake panapo tarehe 31 januari mwaka huu na kuwekwa kwenye matibabu huku akiwa amekosa ufahamu na mpaka kifo chake kumkuta alikuwa hajapata fahamu bado. Inakumbukwa kuwa miaka mitatu iliyopita mama yake Bobbi,alikutwa pia kwenye bafu lake amepoteza fah...

PICHA ZA ZARI AKIWA NA DIAMOND PLATINUMZ MPYA ZAWA GUMZO KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Image
Kwa raha zetu...... vaeni madera, fungeni mikanda mpite kimya kimya Keeping it sexy and classy. #BabyBumpPhotoShoot  CREDIT GOES TO @iviewstudios  and  @raqey_allaraqya

TUJIKUMBUSHE: BOMU LINALOMWANDAMA SAMIA SULUHU HASSAN

Image
Samia Suluhu Hassan Kisiwa cha utalii cha Changuu, kilikodishwa kwa ‘ bei chee’ na kampuni ya Leizure Hotel Limited, ripoti ya Kamati ya Baraza la Wawakilishi (BLW) imebaini. Ripoti ya Kamati ya BLW iliyoundwa kuchunguza ubadhirifu wa mali za serikali , imebaini kuwa kilikodishwa kwa kodi ya Dola 1,000 kwa mwezi na kumtaja aliyehusika na ukodishwaji huo kuwa ni aliyekuwa Waziri wa Utalii Biashara na Uwekezaji Zanzibar, Samia Suluhu Hassan. Waziri huyo wa zamani anatajwa kuwa alishirikiana na Kitengo cha Uwekezaji Zanzibar, (ZIPA) kufanikisha suala hilo Desemba 2002. Katika Baraza la Mawaziri la sasa Samia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano). Kwa mujibu wa ripoti hiyo kisiwa hicho chenye ukubwa wa hekta 11.27 kimekodishwa mwaka 2002 kwa malipo ya Dola za Marekani 1,000 kwa mwezi katika kipindi cha miaka 30. (Dola moja ni karibu sawa na Sh. 1,580) Hata hivyo kodi hiyo imerekebishwa na kufikia Dola 3,500 licha ya kwamba kabla ya kuwamilikisha wageni kisiwa hicho k...

SOMA HABARI ZA MAGAZETI YA LEO JUMATATU, JULY 27

Image