MFANYABIASHARA NDOGODOGO ASHINDA UBUNGE VITI MAALUMU MKOA WA MARA
na shomari Binda
MCHUUZI wa
dagaa kwenye soko la Mwigobero lililopo Manispaa ya Musoma,Agnes Methew,ameibuka
mshindi wa kwanza kwenye kura za maoni za kutafuta Mbunge wa viti maalumu(CCM)
mkoa wa Mara.
Akitoa
shukrani kwa wajumbe wa mkutano wa uchaguzi mara baada ya kutangazwa mshindi na
msimamizi wa uchaguzi huo,Samwer Kiboye ambaye ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Rorya,alisema wajumbe wameonyesha namna ambavyo hata mtu wa chini anaweza
kushinda tofauti na inavyozungumzwa.
Alisema wao
watu ambao wamekuwa wakizungumza pembeni ukiwa Chma cha Mapinduzi huwezi kupata
nafasi ya uongozi kama hauna fedha jambo ambalo sio kweli kwa kuwa yeye
amechaguliwa bila kujali kipato chake na kuwashinda walioonekana na kipato cha
juu na majina makubwa.
“Niwashukuru
sana wajumbe kwa kunipigia kura za kishindo na kunifanya niibuke mshindi kati
ya wagombea wengine 9 wanachma wenzangu ambao nilikuwa nikishindana nao ndani
ya uchaguzi huu.
“2010
nilikuja kwa mara ya kwanza kuwaomba nafasi hii lakini kura hazikutosha lakini
safari hii mmeamua kunichagua mimi muuza dagaa na kuudhilihisha umma ndani ya
CCM hata mtu wa hali ya chini anaweza kupewa uongozi.
Kwa jinsi
mlivyoniamini naomba niwahakikishie
sito waangusha na kikubwa naomba tupeane ushirikiano na pale nitakapofanikiwa
kuingia bungeni nitakuwa mstari wa mbele kuzungumzia masula yanayowahusu
wanawake katika kufanikisha chachu ya maendeleo,”alisema Agnes.
Wakati
akiomba kura kabla ya kuchaguliwa,mgombea huyo aliwatoa chozi wajumbe baada ya
kuomba kura huku akilia akiomba kuchaguliwa muuza dagaa kwa kwa kipindi chote
amekuwa yupo na wajumbe katika kiangazi na mvua.
Katika
uchaguzi huo,Agnes Methew alichaguliwa kwa kupata kura 418 kati ya kura 641
zilizopigwa na kufuatiwa na Chrstina Samo aliyepata kura 226 huku Mwenyekiti wa
(UWT) mkoa wa Mara,Nancy Msafiri akipata kura 208 na kushika nafasi ya tatu.
Awali
akizungumza kabla ya kuanza kwa mkutano huo,msimamizi wa uchaguzi,Samwer
Kiboye,aliwahasa wagombea wote kukubalina na matokeo kwa kuwa uchaguzi ni wa
haki ili kuweza kushirikiana kwa pamoja kutafuta kura za CCM katika kuelekea
uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba.
Comments
Post a Comment