Al Shabaab wadai kuteka askari wa Uganda
Wapiganaji wa Al Shabaab
Wapiganaji
wa kiislamu wa Alshabab wamesema katika maneno yao kuwa linawashikilia
mateka wa kivita kutoka Uganda waliowateka wakati wa mashambulizi ya
wiki iliyopita.
Uganda
imesema kuwa wanajeshi kumi na mbili waliokuwa chini ya jeshi la umoja
wa Afrika wakilinda amani nchini Somalia waliuawa katika shambulio hilo
kwenye ngome yao iliyopo kusini mwa nchi hiyo.
Wanadiplomasia wa nchi za magharibi wamesema kuwa zaidi ya wanajeshi mia moja wa Uganda aidha wamekufa au hawajulikani walipo.
Afisa mmoja wa kundi la Alshabab amesema wanajeshi hao wa Uganda wapo salama na wana afya njema.
Hakuweza kusema ni wangapi walioshilikiliwa ama nini kinaweza kutokea kwa mateka hao.
Amesema Uganda imefanya makosa ilipotamka juma lililopita kuwa wanajeshi wake wote wamehesabiwa.
Katika
siku kadhaa zilizopita wanamgambo hao wa Al Shabaab walitumia picha za
askari waliofariki wa Umoja wa Afrika na vifaa vyao katika kuendeleza
propaganda zao.
Ingawa
kundi hilo hivi karibuni limepoteza maeneo mengi nchini Somalia, juma
lililopita lilikamata miji miwili iliyokuwa iliyoachwa na jeshi la umoja
wa Afrika.BBC
Comments
Post a Comment