MAGUFULI ATIKISA MIKOA YA GEITA NA SHINYANGA
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk Jonh Pombe Magufuli akifanya mkutano wa kampeni katika viwanja vya UWT CCM, Kahama.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Abdalah Bulembo akiwataka wananchi kumchagua Magufuli.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Msitaafu, Samuel Sitta akimnadi Magufuli.
Katibu Mwenezi wa Chadema, Musa Dida akirudisha kadi ya chama chake, kuvua gwanda na kuchukua kadi ya CCM.(P.T)
Sehemu ya wakazi waliofurika katika viwanja vya UWT Kahama wakiwa na mabango ya kumfagilia Magufuli.
Wakazi wa kijiji cha Bulungwa wakimsikiza Magufuli baada ya kumsimamisha barabarani
Wakazi wa kijiji cha Igulwa
Wakazi wa Mbogwe wakimsikiliza Magufuli
Wakazi wa mgodi wa Nyarugusu
Kundi la waimbaji wa Yamoto Bendi wakifanya yao viwanja vya UWT Kahama.
Mgombea
urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Dk John Pombe Magufuli leo ameitikisa mikoa ya Mikoa ya
Geita na Shinyanga kwa kufanya mikutano 14 ya kampeni katika maeneo
tofauti .
Dk
Magufuli alifanya mikutano katika vijiji saba vya mkoa wa Geita na
mikutano mingine saba aliifanya mkoani Shinyanga ukiwemo mkutano
uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi kwenye viwanja vya UWT CCM vilivyopo
Kahama Mjini.
Katika
kampeni hizo wanachama zaidi ya 20 kutoka vyama pinzani vya siasa
vinavyoshiriki uchaguzi Mkuu walisalimisha kadi zao kwa Magufuli na
kujiunga CCM. Wanachama hao waliahidi kumuunga mkono Magufuli kwa kumpa
kura zao urais pamoja na wabunge na madiwani wa CCM.
Katika
kampeni zake ambapo leo Magufuli kakribani maeneo yote aliyofanya
mikutano yanawahusu wachimbaji wa madini. Magufuli aliwaahidi neema
wachimbaji hao kuwa, endapo watamchagua na kufanikisha kuwa rais wa
Tanzania, atawamilikisha machimbo mapya watakayovumbua.
Kuhusu
wafugaji katika maeneo hayo, Magufuli aliwaahidi kuwatafutia wawekezaji
wa viwanda vya ngozi ili kupandisha thamani ya mifugo yao. Aidha
Magufuli aliwaambia wakulima wa pamba kuwa, endapo watamchagua yeye,
madiwani na wabunge wa CCM, ataanzisha viwanda vya nyuzi na vitambaa
hivyo akawataka wananchi hao wakae mkao wa kimaendeleo.
Mgombea huyo leo kampeni zake ziliishia uwanja wa UWT CCM Kahama Mjini ambapo kesho zinatarajia kuishia Shinyanga Mjini.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS/GPL ALIYEKO SHINYANGA)
Comments
Post a Comment