Taarifa kutoka HESLB: Ofisi zitakuwa wazi Jumamosi na Jumapili hii
Taarifa kutoka HESLB: Ofisi zitakuwa wazi Jumamosi na Jumapili hii BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU TAARIFA KWA UMMA OFISI ZA BODI YA MIKOPO KUWA WAZI KESHO JUMAMOSI NA JUMAPILI Bodi ya Mikopo inapenda kuwataarifu wadaiwa wote waliopo Dar es Salaam kuwa Ofisi za Bodi zitakuwa wazi kwa siku mbili za kesho, Jumamosi, Julai 30, 2016 na Jumapili, Julai 31, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 9:00 mchana ili kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kuwasiliza wadaiwa. Hii ni fursa muhimu kwa wadaiwa wote wa mikopo ya elimu ya juu ambao hawajaanza kulipa mikopo kupata taarifa kuhusu madeni yao. Bodi ya Mikopo inatarajia kuanza kuwachukulia hatua za kisheria wadaiwa wote ambao hawataanza kulipa madeni yao mara moja. Hatua hizo ni pamoja na: i. Kufikishwa mahakamani; ii. Kutozwa faini; iii. Kunyimwa fursa za kupata mikopo; iv. Kunyimwa fursa za masomo nje ya nchi; na v. Kuzuiwa kusafiri nje ya nchi. Nyote mnakaribishwa ili kutumia fursa hii muhimu. Imetolewa na: Bw. Jerry Sa...