KADI ZA VISA ZA BANCABC KUPUNGUZA WIZI WA PESA
Mkuu wa
Kitengo Cha wateja binafsi na wafanya baishara wadogo wa BancABC, Bi
Joyce Malai akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa
uzinduzi wa kadi ya VISA ya BancABC maalum kwa wateja wao na hata wasio
wateja wao. BancABC imezindua kadi hiyo ya Visa ili kupunguzia wateja
adha kubwa ya kubeba fedha tasilimu wanaposafiri ndani na nje ya nchi.
hafla ya uzinduzi ilifanyika jana viwanja vya sabasaba
Mkuu wa
Masoko wa BancABC, Bi Upendo Nkini, akielezea faida za kadi Mpya ya VISA
ya BancABC inayomwezesha mteja kufanya malipo ya mtandaoni kwa urahisi
kwa kuwa kadi hiyo inalindwa kwa kutumia teknolojia mpya ya CHIP na PIN.
Wafanyakazi
wa BancABC kitengo cha huduma kwa wateja Bw, Ally Miraji kushoto na Bi
Neema David wakimuhudumia mmoja wa wateja aliyekuwa akichukua kadi ya
VISA ya BancABC bw, Fredrick Israel katika banda la Bank hiyo viwanja
vya sabasaba. BancABC imezindua kadi hiyo ya Visa ili kupunguzia wateja
adha kubwa ya kubeba fedha tasilimu wanaposafiri ndani na nje ya nchi na
kwamba ni njia bora ya kufanya malipo kupitia mitandao kwa kuwa
imeunganishwa na mitandao ya simu kama Airtel Money, TigoPesa, na Mpesa.
mteja ili kupata kadi hiyo sio lazima awe na akaunti ya BacABC. hafla
ya uzinduzi ilifanyika jana viwanja vya sabasaba
Wafanyakazi
wa BancABC kitengo cha huduma kwa wateja Bw, Ally Miraji kushoto na
wenzake wakitoa huduma ya maelekezo kwa bw, Ahmad Ibrahim kuhusu
matumizi ya kadi mpya ya VISA ya BancABC katika viwanja vya sabasaba.
BancABC
imezindua kadi hiyo ya Visa ili kupunguzia wateja adha kubwa ya kubeba
fedha tasilimu wanaposafiri ndani na nje ya nchi na kwamba ni njia bora
ya kufanya malipo kupitia mitandao kwa kuwa kadi hiyo imeunganishwa na
mitandao ya simu kama Airtel Money, TigoPesa, na Mpesa hafla ya uzinduzi
ilifanyika jana viwanja vya sabasaba.
Kadi ya VISA ya BancABC ndio kadi pekee inayohudumia wateja wa huduma za fedha za mitandao ya simu.
BancABC,
ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imekuja na tiba ya kukithiri kwa wizi wa
pesa ambao husababishwa na baadhi ya watu kuzunguka na fedha nyingi
mifukoni mwao kwani imeanzisha kadi mpya ya Visa ambayo itaweza kujazwa
pesa kwa kutumia shilingi ya Tanzania, Rand ya Afrika Kusini, Dola ya
Kimarekani, Euro na Pauni ya Uingereza.
Akizungumza
Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo Cha wateja binafsi na wafanya
baishara wadogo, Bi Joyce Malai alisema kadi hiyo itaweza kutumiwa na
wateja walio na wasio na akaunti za BancABC na kwamba itawapunguzia adha
kubwa ya kubeba fedha tasilimu wanaposafiri nadani na nje ya nchi na
kwamba ni njia bora ya kufanya malipo kupitia mitandao.
Alisema
watatumia maonesho ya Saba Saba kuitangaza kadi hiyo na wateja wataweza
kupata kadi ndani ya muda mfupi baada ya zoezi fupi la usajili ambalo ni
papo kwa papo. “Ukiwa na kadi hii utaepuka usumbufu mkubwa mno kwani
huhitaji kubeba fedha tasilimu na pia sio lazima uwe na akaunti ya
benki,” alisema.
Alisema
watumiaji wataweza kupata huduma masaa 24, siku saba kwa wiki mahali
popote kupitia ATM zaidi ya 400 zenye huduma ya Visa nchini Tanzania
ambapo ATM za aina hii zinafikia milioni 1.3 duniani na pia watumiaji
wanaweza kufanya miamala kwa watoa huduma zaidi ya 1000 Tanzania na
zaidi ya milioni 35 duniani kote.
“Tumepata
ushuhuda na mrejesho mzuri kutoka kwa wateja wetu ambao wana watoto
wanaosoma nje ya nchi kwani wanaweza kuwatumia fedha za kujikimu kila
mwezi bila kuingia gharama za ziada,” alisema.
“Kinachofaya
kadi hii ya Visa iwe ya kipekee ni pale ambapo mteja anaweza kuweka
fedha kwenye kadi kwa kutumia huduma ya kutuma pesa kupitia simu ya
mkononi yoyote na tunajivunia kuwa benki yetu ndio yenye huduma hii
pekee kwa sasa,” alisema.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Masoko, Bi Upendo Nkini, faida nyingine za kadi hiyo
ni kama vile kufanya malipo ya mtandaoni kwa urahisi zaidi, kuthibiti
matumizi kwani utatumia kiasi cha fedha kilichoko kwenye kadi pekee na
pia kuwa na amani kwani pesa zinakuwa salama kwani kadi inalindwa kwa
kutumia teknolojia mpya ya CHIP na PIN.
Alisisitiza
kuwa hii ndio kadi pekee ya Visa Tanzania ambayo unaweza kutumia kwa
ruzuku tano ambazoni shilingi ya Tanzania, Rand ya Afrika Kusini, Dola
ya Kimarekani, Euro na Pauni ya Uingereza na kwamba kadi hiyo, ambayo
inaweza kutolewa kwa mtu kama zawadi, inaweza kutolewa nyingine pindi
inapoibiwa au kupotea.
“Kadi
hizi zitapatikana katika banda letu lililoko katika maonyesho ya Saba
Saba Ukumbi wa Kimataifa lakini pia unaweza kutuma ujumbe mfupi wenye
neno VISA ikifuatiwa na Wilaya uliyopo , kwenda namba 15774,” alisema.
Atlas
Mara iliinunua BancABC in Juni 2014 huku ikizidi kujitanua Tanzania, ,
Botswana, Mozambique, Zambia na Msumbiji. Baada ya hapo ilinunua benki
mbili nchini Rwanda (BR Commercial na BPR ambazo zinaendelea kukamilisha
mchakato wa kuungana).
Comments
Post a Comment