YOUNG D AZUNGUMZIA MAMBO 6 KATIKA KIPINDI CHA MKASI JANA

.
.
Kama hukuwa karibu na TV yako kuangalia show ya Mkasi on EATV November 17 2014 usiku haya ni mambo sita aliyoyazungumzia Rapper Young Dee kuhusiana na tatoo zake, anachikofikiria kukifanya kama akiacha muziki, msichana aliyemwimbia “Siyo mchoyo’, kukopi style ya muziki na kuhusu yeye na shule.
Mtangazaji Salama Jabir na timu yake ndio wameongoza maswali kwa Young Dee.
.
.
Salama: “… Mara yako ya kwanza kuchora tatoo ulikuwa una miaka mingapi?…”
Young Dee   : “…Actually sikumbuki nilikuwa na miaka mingapi.. lakini ilikuwa ni kipindi ambacho nilikuwa nimeanza kuandaa albam yangu inaitwa ‘The City of David’ .. tatoo yangu ya kwanza imeandikwa ‘The City of David’.. hii ndiyo project ambayo ninaifanya hadi sasa hivi kuanzia  kwenye ‘dada anaolewa’.. ‘tunapeta’ .. hadi sasa hivi nyimbo zangu zinazotoka ni project ambayo nimeanza kuifanya muda mrefu.. nina kama miaka mitano kama sikosei kwa  hiyo miaka mitano iliyopita ndio nilichora tatoo yangu ya kwanza….
Salama          : “..Wewe kwa jinsi ulivyo, unadhani utafanya muziki maisha yako yote, kwanza.. cha pili, kama  ukiamua kuacha muziki na kufanya kitu kingine pengine kufanya kazi Bank, ama UN, ama wherever..  hauhisi kwamba maamuzi yako ambayo unayafanya sasa hivi yanaweza yakakugharimu kwa vitu vya baadaye…?”
Young Dee   : “…. Sijawahi kufikiria kufanya kazi UN au Bank wala nini.. wala kuwa mwanajeshi..  Sijawahi kufikiria hivyo, wala sitamani.. Wala sita-enjoy na sitapenda na siwezi kufanya kitu ambacho sikipendi, lazima nifanye kitu ambacho nakipenda.. hata ikibidi hakinilipi kabisa kama nakipenda, naenjoy kukifanya then I will do it mpaka nitakapofariki….
Muba             : “…Ule wimbo umetoa juzi unaitwa siyo mchoyo, nimesikia baadhi ya watu wanaongea kwamba kweli kuna demu ambaye kabisa yupo, ni ukweli kwamba ulimwandikia demu yoyote?…
Young Dee   : “… Huyo demu ndiyo yupo.. yupo.. siyo mchoyo kweli.. mimi hata sikuutunga sana yaani..  kwa sababu nimechoka kutunga siku hizi naongea kitu ambacho nakiona…
Muba             : “..Wanasemaga Young Dee anacopy sana style yani unasikiliza nyimbo za akina Lil Wayne halafu unakuja kuchukua style katika mashairi ya mtu..?”
Young Dee   : “… Sijawahi kuchukua mashairi ya mtu.. kusikiliza ni kweli mimi nasikiliza kwa sababu mimi muziki kwangu ni maisha yangu.. lazima nisikilize muziki, usinichagulie nini cha kusikiliza…
Salama          : “… Wewe ni kijana na umeanza kufanya kazi muda mrefu sana.. niambie shule yako ikoje…?”
Young Dee  : “… Nimeishia O Level, mambo ya kifamilia nikashindwa kuendelea tena so ikabidi nitafute ugali kwa style nyingine.. ndiyo ikawa hivyo.. bado nafikiria kurudi shule lakini nitakapojua nini nakitaka shuleni.. nikishaweka akili yangu hivyo, then nitarudi shule…
.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA