DR SLAA: vichwa vyetu vina TATIZO
Katibu Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) DR Wilbrod Slaa, ameitaka serikali
kuwaeleza wananchi ukweli kuhusu hali mbaya ya kifedha ambayo
inalikabili taifa hivi sasa kwa kupungua kwa mapato ya ndani na ya nje,
ikilinganishwa na bajeti iliyopitishwa kufafanua mkakati wa kuongeza
uzalishaji na kupunguza matumizi ya serikali.
Kwenye sentensi nyingine,
Dr slaa ameitaka CCM, serikali na vyombo vya dola kubadilika 2012 ili
kuepusha nchi kuingia katika malumbano na migogoro ya kijamii, ambapo
ishu nyingine aliyoizungumzia baada ya kukutana na waandishi wa habari
leo jijini Dar es salaam, ni kuitaka serikali kushughulikia chanzo cha
matatizo ya wananchi, na sio kushughulikia matawi ya matatizo hayo.
Hakusahau kuzungumzia
ishu ya wakazi wanaoishi mabondeni dar es salaam, ambao zaidi ya siku 10
zilizopita, walikumbwa na mafuriko yaliyopoteza maisha ya zaidi ya watu
40, ambapo amesema “ni aibu juzi TABATA ndege
ya polisi inapita badala ya kuokoa watu, inakagua tu na kuondoka, VICHWA
VYETU VINA TATIZO, rais anasema wenye nyumba watafidiwa, je na wale
wapangaji? wamepoteza mali na watoto….. hii ndio aina ya serikali
tuliyonayo, kama tunaweza kuweka mabomu makubwa ya kuwapiga kina Dr Slaa
tunashindwa kununua vifaa kama helkopta na boti za kuokoa rais?
serikali inatakiwa kushughulikia chanzo cha matatizo” – DR SLAA
this is t bro iwould like to share ideas throu my blog gmarandu.blogspot.com
ReplyDelete