Serikali yarejesha mtihani wa Kitaifa Kidato cha Pili kuanzia mwaka huu


Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillipo Mulugo (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam
Baada ya kuifuta kwa miaka kadhaa, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Mafunzo na Ufundi imetangaza kuirejesha tena hadhi ya mtihani wa Kitaifa kwa kidato cha pili kwa shule zote za Sekondari za binafsi na serikali.

Mitihani hiyo inaanza kufanyika rasmi mwaka huu wa 2012 lengo likiwa ni kuthaminisha kiwango cha elimu kwa wanafunzi na utoaji wa elimu kwa shule husika.

Mwanafunzi atakayepata wastani wa asilimia 30 au chini ya hapo, hataruhusiwa kuendelea na masomo ya kidato cha tatu lakini ataruhusiwa kukariir darasa kwa mwaka mmoja tu. Ikiwa mwanafunzi huyo atafeli kwa kushindwa kufikia wastani uliotajwa hapo awali, mwanafunzi huyo ataeondolewa kabisa katika mfumo rasmi wa elimu.

Naibu Waziri wa Elimu, Philipo Mulugo amesema, "...mtihani huu ni tathmini ya kati, inayopima kiwango cha maarifa na ujuzi alioupata mwanafunzi kutokana na masomo aliyojifunza katika kidato cha kwanza na wa pili. Mtiahani wa kidato cha pili ni njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa, wadau wote wakiwemo wazazi, wanafunzi na waalimu wanawajibika ipasavyo katika utoaji wa elimu ambapo kwa kufanya hivyo, tutapata wanafunzi wazuri na ili kujiwekea misingi bora ya uanafunzi katika ufunzaji."

Bwana Mulugo akasema kuwa Wazazi na Walezi watapaswa kugharimia uendeshaji wa mtihani huo kwa kuchangia Tsh. 10,000 na mingine ya kitaifa ya kidato cha nne na sita ni Tsh. 35, 000 kwa mwaka huu.

Amesema sababu mojawapo ya kiuchunguzi kufuatia kufeli kwa wanafunzi mwaka 2010 katika mtihani wa Kitaifa ilionesha kuwa kutokufaulu kulichangiwa kwa kuwaruhusu wanafunzi kuendelea na masomo hata baada ya kushindwa kufikia alama za ufaulu.

Vile vile Mulugo alisema Serikali inararjia kutangaza ajira za walimu wa msingi na sekondari mwezi huu , na hivi karibuni itatangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha pili.

Hii ni ni mara ya pili kwa serikali kurejesha mtihani wa kidato cha pili mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1999 tangu ulipoanzishwa mwaka 1984. 
Picture
Mkurugenzi wa Shule za Sekondari, Charles Philemon akifafanua jambo

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA