Somo toka RITA: Elimu juu ya Taratibu za kuandika wosia

TARATIBU ZA KUANDIKA WOSIA Taratibu za kuandika wosia zinatofautiana kulingana na sheria ya mirathi inayotumika. 1. WOSIA WA MAANDISHI Wosia huu unashuhudiwa na watu wawili pale ambapo mtoa wosia anajua kusoma au kuandika. Shuhuda mmoja lazima awe ndugu wa karibu wa mtoa wosia na mwingine ambaye sio ndugu wa karibu.Wosia na unatakiwa uwe na tarehe, uandikwe kwa karamu ya wino au upigwe chapa na uwe na saini ya mtoa wosia na saini za mashuhuda ambapo wote wanatakiwa kutia saini zao kwa wakati mmoja. Mtoa wosia asiye jua kusoma ua kuandika awe na mashuhuda wa nne wanao jua kusoma na kuandika,muhusia huyo aweke alama ya kidole gumba cha mkono wake wa kulia,mashuhuda hao wote washuhudie na waweke saini zao kwenye Wosia kwa wakati mmoja. 2. WOSIA WA MDOMO/MATAMSHI Wosia huu unashuhudiwa na mashuhuda wasiopungua wa nne wawili kati yao ndugu wa mtoa wosia na wawili waliobaki wasio ndugu wa mtoa wosia.Wosia huu utolewa na mtu asiye jua kusoma na kuandika. TARATIBU ZA KUANDIKA WOSIA KATIKA SHERIA ZA MIRATHI Wosia katika Sheria za kimila,zipo katika jedwali la 3 la Sheria ya (The Local Customary Law (Declaration|) No. 4 Order, 1963. Wosia katika Sheria za kiserikali, zipo katika sheria iliyorithiwa kutoka kwa Waingereza ya (The Indian Succession Act ), iliyopitishwa huko India mwaka 1865. Hauna tofauti kubwa na wosia wa kimila isipokuwa wosia huu unatakiwa uwe katika maandishi. Vipengele vyote vya wosia wa maandishi vinatumika. Mtoa wosia anaweza kufuta au kuongeza maneno mengine kwa kuandika maandishi mengine ambayo yatatakiwa kuzingatia masharti ya uandikaji wosia. Wosia katika Sheria za kiislamu, mtoa wosia anaruhusiwa kuuusia 1/3 ya mali yake 2/3 lazima irithiwe na warithi halali. source www.wavuti.com

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA