UDA-RT kuanza kuuza hisa mwezi Machi
Robert Kisena MWENYEKITI wa Kampuni ya Simon Group, Robert Kisena, amesema UDA-RT imewekeza zaidi ya Sh bilioni 90 na kuanzia Machi mwaka huu kuna mpango wa kuanza kuuza hisa kwenye Soko la Hisa. Pamoja na hali hiyo kampuni hiyo imeweka wazi wamiliki halali wa UDA wanaotambulika kwa mujibu wa sheria. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam jana kuhusu tuhuma kwamba Kampuni ya Simon Group ilipata upendeleo kununua Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), pamoja na kutoa ufafanuzi wa wanahisa halali kwa mujibu wa sheria. Alisema hivi sasa kampuni hiyo imejikita katika kuhakikisha Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi, unaanza kwa wakati sambamba na uuzaji wa hisa. Kisena alisema kuna mpango wa kuuza asilimia 70 ya hisa zake kwenye soko la hisa. “Tunatarajia kupata Sh bilioni 600 ambazo zitatumika kujenga maegesho ya magari ambayo yatakuwa na huduma nyingine kama maduka na kadhalika,” alisema Kisena. Alisema wamiliki wa mabasi 138 ya dalalal